VIWANDA VYA SUKARI KUJENGWA KIGOMA, RUVUMA NA TANGA - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Monday, November 2, 2026

VIWANDA VYA SUKARI KUJENGWA KIGOMA, RUVUMA NA TANGA


NA MWANDISHI WETU


VIWANDA vya sukari vitatu viko katika mchakato kujengwa nchini jambo litakasaidia kupatikana kwa bidhaa hiyo kwa wingi nchini.


Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uwekezaji   na Maeneo Maalum ya  Kiuchumi Tanzania, (TISEZA), Gilead Teri, amesema kwamba viwanda hivyo vinajengwa katika eneo la Kasuru mkoani Kigoma, Mshindo Songea mkoani Ruvuma na kingine kinajengwa Pangani mkoani Tanga.

Hayo amezungumza leo jijinj Dar es Salaam wakati akizungumza na wahariri na waandishi wa vyombo mbalimbali nchini katika kikao kazi kilichiandaliwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina.

"Naamini viwanda hivyo vikikamilika suala la utoshelezi wa sukari nchini litakwenda kuwa la uhakika na ifikapo mwaka 2028 vitakuwa vimeanza uzalishaji," amesema.


Akizungumzia sekta inayoongoza katika uwekezaji nchini amesema ni viwanda inashika nafasi ya kwanza ikiwa na miradi 1650, Uchukuzi ikiwa na miradi 525, Ujenzi Majengo ya kibiashara ikishika nafasi ya tatu ikiwa na miradi 361 na nafasi nne ikishikwa na sekta ya Utalii ikiwa na miradi 338.


Aidha amesema mikoa inayofanya vema kwenye uwekezaji hadi sasa ni Dar es Salaam yenye miradi 1339, Pwani inashika nafasi ya pili ikiwa na miradi 680, Arusha inashika nafasi ya tatu ikiwa na miradi 232, Mwanza inashika nafasi ya nne ikiwa na miradi 164 na nafasi ya tano inashikwa na Dodoma ikiwa na miradi 157.


Pia Teri, ameongeza kwamba mchakato unaendelea kufanyika kuhamasisha ili kuhakikisha 2027 Dodoma inaongoza kwenye sekta ya viwanda na anawakabirisha wawekezaji kwenda kuwekweza katika eneo la Nala lenye ekari 500 na zinamiundombinu ya kutosha kufanikisha hilo.








No comments:

Post a Comment