Na Magendela Hamisi
“Nilivutiwa na Shadya Mohamed ambaye aliwahi kuwa miss Kanda ya Nyanda za Juu na alifanikiwa kushiriki kinyang’anyilo cha kumtafuta miss Tanzania na nikaanzia katika katika mashindano ya Kitongoji cha bagamoyo Miss Bagamoyo”, alisema Thureya Damas.
Miss huyo ambaye kwa sasa akiwa katika maandalizi ya kuingia kambini mkoani morogoro katika kuwania taji la Miss Kanda ya Mashariki akiwa na imani ya kuibuka mshindi wa kanda hiyo inayoshiriksha mikoa ya pwani, Mtwara,Morogoro na Lindi.
Anasema tangua aanzea kushiriki Mashindano hayo ngazi ya Kitongoji amekutana na ameshakabiliana na changamoto mbalimbali ambazo zingine zilimkatisha tamaa lakini kutokana na uvumilivu wake aliweza kuzishinda na hatimaye kufikia katika hatua hiyo.
Thureya kwa sasa akiwa ni mwanafunzi wa Chuo cha Uandishi wa Habari kiwango cha Stashahada, anasema anauzunishwa na fani hiyo inavyoingiliwa na watu wasiokuwa na taaluma hiyo ambao kwa namna moja au nyigine wanakuwa wakiipeleka pabaya taaluma hiyo na kufanya kudhaurika .
Hivyo anawaomba watu wasiokuwa na taaluma ya habari na kuhitaji fani waende shule ili waweze kufahamu misingi ya taaluma hiyo na kuwataka wale walio elimu ya hiyo wafuate taratibu za uandishi na kuwa na kumbukumbu katika kazi zao za kila siku.
Baada ya fainali ya ya kitongoji cha Bagamoyo Dabas alifanikiwa kutwaa taji la kitongoji na kuwa mwanzo wa mafanikio yake katika tasnia hiyo ambayo kwa namna moja au nyingine na kufanikiwa kuingia katika fainali ya Mkoa wa Pwani.
Katika mashindano hayo ya mkoa wa Pwani alifanikiwa kushika nafasi ya pili kati ya 13 na kupata nafasi ya kushiriki katika fainali ya Kanda ya Mashariki na akiwa na matumaini makubwa ya kufanya vizuri katika kinyanganyilo hicho na kuapata nafasi ya kuiwakilisha kanda hiyo katika mashindano ya Miss Tanzania .
Anasema ikiwa atafanikiwa kutwaa taji la kanda ya mashariki na kupata nafasi ya kuiwakilisha katika miss Tanzania, Vodacom 2011/2012 na ikiwa atafanikiwa kupata taji hilo la Vodacom Miss Tanzania atakuwa pamoja na jamii ili kuweza kujua matatizo yao na kuwasaidia.
Dabas ni aliitimu elimu ya Msingi katika Shule ya Bilal Comprihensive mwaka 2003, iliyopo Dar es Salaam kumalizia elimu ya kidato cha nne katika shule ya Jamhuri , Dar es Salaam mwaka 2007.
Anasema hadi sasa ana matumaini makubwa ya kufanikiwa kuchukua umalikia wa kanda ya Mashariki inayotarajiwa kufiia ukikongoni Julai 22 mwaka huu mkoani Morogoro kutokana na maandalizi aliyoyafanya ili kuweza kuchukua taji hilo Baada ya kuingia kambini Julai 18 mwaka huu.
Mnyange huyo mwenye makeke mengi awapo jukwaani kupanda jukwaani akipambana na Wanyange wengine 20 wanaowania taji la Kanda la Mashariki ambapo akijjnasibu kwa kujiamini alisema kuwa ahofii uwezo wa washiriki wenzake na kuona kuwa ni wakawaida ukilinganisha na wale aliokutananao katika vitongoji.
“Siofii uewzo wa wezangu kutokana na kuwasoma kwa kipindi hiki, kwa muda mfupi nimeona mapungufu yao , hivyo nitatumia nafasi kufanya vyema na kufanikisha ndoto yangu ya kuchukua taji la miss Tanzania .” Alisema Dabas.
Alisema alipita katika vikwazo vingi hadi kufika katika hatua hiyo, hivyo kutokana vikwazo alivyokutana navyo anaamini atafanya vyema na kunyakua taji hilo .
Naomba mungu na mashabiki wangu waniombee kwa mungu ili niweze kufany vizuri karika mashuimdano ili niweze kufanya vizuri na niweze kuwawakilisha vyema katika mashindano yaMiss Tanzania na Miss Wolrd.




No comments:
Post a Comment