Na Hamisi Magendela
Katika michuano ya Kombe la Kagame iliyomaliziki Julai 10, na timu ya Yanga kutawazwa kuwa mabingwa wapya wa michuano hiyo baada ya kuiwatandika maasimu wao Simba kwa bao 1-0.
Vijana hao jangwani waliweza kubeba ubingwa huo wakiwa wanatokea katika adhabu ya kutoshiriki michuano hiyo kwa miaka mitatu na wakiwa wametumikia kwa miaka miwili baada ya kuomba radhi na kukubali kulipa dola marekani 20,000 ikiwa ni adhabu ya kutoingia uwanja wakati wa mechi yao ya kutafuta mshindi wa tatu dhidi ya Simba mwaka 2008 katika uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Katika michuano hiyo mashabiki lukuki walikuwa wakiingia zaidi wakati timu zao za nyumbani Simba na Yanga zikicheza na kuonesha uzalendo wa kwenda kuzishangilia kwa nguvu zote kuhahakisha zinapata ushindi wa kuwawezesha kusonga mbele katika mashindano Mashindano hayo.
Ukweli jitihada za mashabiki hao ziliweza kuhamasisha timu hizo kufika fainali ya aina yake na watazamaji 53,000 waliiingia kushuhudia fainalia ya kiistoria ikifanyika kwa aina yake.
Na fainali hiyo ilikuwa ya kiistoria kutokana na kuwakutanisha mahasimu wawili kutoka nchi moja ya ukanda wa Afrika Mashariki na Kati na pia kukatika kwa umeme wakati wa kukabidhi zawadi hasa kwa Mabingwa wa michuano hiyo, hiyo ni historia.
Kikubwa ninachotaka kuzungumzia ni kuhusu Askari wetu ambao wanaaminika kuwepo uwanjani kwa suala la ulinzi na kuangalia mpira kama wanavyofanya askali wetu.
Katika mashindano ya Kombe la Kagame na mashindano mengeni askali wengi wamekuwa na tabia ya kukaa katika viti na kuanza kuangali mpira na kuwanyima wale waliotoa fedha zao wakiwa wamesimama.
Wengine hawaishii hapo wanakwenda mpaka na redio ndogo wakiziweka masikioni kwa na kufutilia mpira kwa makini na wakiacha suala la ulinzi likiwa halina mwenyewe.
Hii ni hatari ambayo endapo haitazibitiwa mapema itakuja kuleta madhalamakubwa nan pengine maafa kwa maana wanaoingia kutazama mchezo wa mpira wa miguu wanakuwa na mapenzi tofauti ya timu husika.
Pia mashabiki wengine wanakuwa ndiyo ndiyo mara yao ya kwanza kuingia uwanjani kushuhudia mchezo huo na mara nyingi zinapocheza Yanga na Simba ambao ni mahasimu wakubwa na endapo mshambiki bila ya kufahamu akaingia upande wa mashabiki wa pande akaingia sehemu hasiyo husika matatizo makubwa yanaweza kumkuta na wakati Askali hayuko kwa ajili ya kuangali ulinzi, hivi unafikili nini kitamkuta?.
Pia kutokana na askali hao kutokuwepo na hali ya kuangalia ulinzi madhara makubwa yakiwemo maafa kwa maana mpaka askali wafahamu kuwa kuna mtu anafanyiwa uovu ni muda mwingi utakuwa umepita na madhara makubwa yamekwishatokea.
Ni vyema tukaelezwa kama askali hao wapo kwea ajili ya kuangalia usalama au wanaingia uwanjani kwa ajili ya kuangalia mpira ikiwa ni hivyo na wao wachajiwe kiingilio kama masahabiki wengine.
Kibaya zaidi askali hao wanakuwa wakishangilia mara tu bao linapofungwa kitu ambacho kinatufanya tushindwe kuelewa kama kweli wapo uwanjani hapo kwa ajili ya kuangalia usalama wa mashabiki na mali zao au kuangalia Mpira.
Na wengine wanakuwa wakibishana kuhusu mchezo unavyoendelea na masahabiki kitu ambacho kinakwenda kinyume na taratibu zinavywataka wawepo uwanjani.
Marcus Mpangala ambaye nj miongoni mwa wachambuzi wa soko, anasema askali kwa kufanya hivyo wanafanya makosa na kwa bahati, Tanzania aina mashabiki wenye tabia ya chafu kiasi cha kuleta fujo na kusababisha maafa.
“Tushukuru mashabiki wa kitanzania hawana fujo kiasi kinachoweza kuahatarisha amani kwenye uwanja, wana upendo na wanavumiliana kwa asilimia kubwa kuliko na mashabiki wan chi nyngine,hivyo napenda kuwashauri askali wetu wafuate kile kilichowapeleka kwa maana siku hazifanani”, alisema Mpangala.




No comments:
Post a Comment