ahadi ya Five Star itekelezwe - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Thursday, September 22, 2011

ahadi ya Five Star itekelezwe

Na Hamisi Magendela
NASIKIA kigugumizi, majonzi namasikitiko makubwa kuona vijana ambao
kwa namna moja au nyingine wakianza kunyanyuka baada ya kupata pigo
kubwa ambalo haliwezi kusahaurika vichwani mwao.
Upweke unaonekana kutawala katika mazoezi, kitu kinachoaminika
kuhamisha kambi yao ya mazoezi kutoka Temeke hadi Ilala, inawezekana
lengo ni kuhepusha hali ya majonzi wa kuendelea na shughuli zao za kila
siku.
Suala la kuhama kutoka sehemu moja kwenda nyingine baada ya msiba
mzito, uwatokea watu ambapo tuliweza kushuhudia hata baadhi ya familia
baada ya kufiwa na mtu wao wa karibu uhama eneo hilo na kwenda
kuendelea na maisha sehemu nyingine.
Lengo la kufanya huvyo inawezekana kuhepusha hali ya kuamini kuwa
wakati shughuli zikiendelea inawezekana hisia ya kutokea kwa mtu huyo
zikajitokeza kitu kinawapa hali ngumu watu mbalimbali na badala yake uona
na heli kuondoka eneo hilo.
Mfano, baada ya Tanzania kupata msiba mzito wa kufariki kwa aliyekuwa
Waziri mkuu wakati huo  marehemu Edward Sokoine, baadhi ya wabunge
inaaminika walikuwa wakihisi kumuona akiingia bungeni kushughulika na
taratibu za bunge, hizi hisia ambazo zinawasumbua watu wengi.
Machi 21mwaka huu, ni siku ambayo bendi ya muziki wa taarabu ya Five
Star, "Watoto wa Bongo" iliwapoteza baadhi ya tegemeo wa bendi hiyo
pamoja na vyombo vyao  vya muziki katika ajali ya gali iliyotokea Mkoani
Morogoro wakiwa wanatoka Iringa katika maonesho yao ya kawaida.
Kipindi kile wadau mbalimbali walijumuika na wafiwa na kuwafariji
kutokana na msiba mzito uliotokea katika tasnia ya mziki wa taarabu na
wengi waliamini kuwa huo ndiyo mwisho wa Five Star "Watoto wa Mjini."
Kwa hali hiyo Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, vijana na Michezo, 
Fanela Mukangala,  alitoa ahadi kwa Viongozi wa bendi hiyo kuwa
watawanulia vyombo vya muziki ili kuweza kuwafanikisha kuisuka benfi
hiyo upya, lakini mapaka sasa hakuna kinaelezwa kinachoendelea wakati,
bendi hiyo inaanza shughuli zake za kutoa burudani.
Ninachouliza......?  iko wapi ahadi walioahidiwa na Serikali kupitia wizara
yake ya Utamaduni, Vijana na Michezo ya kuwanunuliwa vyombo vya
muziki hao ? au ndiyo changa la macho?
Kwa maana hadi leo hakuna lolote linaloelezwa tangu ahadi hiyo ilipotolewa
kwa watoto hao wa Mjini, kintu kinachoonekana ni dangany toto kwa yatima
hao ambao walipoteza wasanii pamoja na vyombo vyao na kuchwa yatima
wakiwa hawajui pa kuanzia.
Kulikuwa na haja gani kutoa ahadi ambayo ilikuwa kwao ni vigumu
kutekelezwa? au alikuwa anafulahishwa nani? naamini hawakuomba ila
kutokana na hali waliyonayo Serikali kupitia Naibu wa Wizara hiyo iliona ni
vyema watu hao wakasaidiwa ili kuweza angalau kuwainua hapo walipo.
Na kila mtu aliamini kuwa jambo hilo lingetekelezwa mapema, lakini mpaka
bendi hiyo inaanza shughuli zake hakuna msaada wa Serikali walioupata kitu
ambacho kinatia shaka, kama baba anatoa ahadi za uongo kwa watoto
aliowazaa, sijui tujifunze nini.
Lakikni pia muda bado upo ni vyema Wizara husika ikajpanga na kuhakikisha
wanawapatia vyombo walivyo wahaidi kwa maana siku zote tunaamini ahadi
ni deni, Pia sipendi kutumia manene yenye ukakasi katika kukumbusha hilo,
kutokana aliahidi ni mtu timamu na hakuwa na haja ya kujipatia sifa zisizo za
masinmngi mbele ya umati uliokuwepo siku hiyo.
Bendi hiyo kwa sasa inatarajia kufyatua nyimbo sita ambazo licha ya kuwa
katika kipindi kigumu wameweza kujipanga na kuhakikisha inainuka vizuri
katika tasnia ya muziki huo, hili ni jambo la kuwapongeza kwa jitihada zao
za kufanukisha suala hilo.

No comments:

Post a Comment