Na Hamisi Magendela
Ajali nyingi zimekuwa zikitokea maeneo mbalimbali nchini na jitihada nyingi zimekuwa zikifanyika kuhahakikisha ajali zinapungua ili kunusuru maisha ya watui na mali zao.
Katika baadhi ya maeneo jijini dare s Salaam kutokana na ajali kuongezeka katika maeneo Halmashauri ya jiji iliona ni vyema kuweka uzio ili kunusuru watu kuendelea kupoteza maisha katika maeneo.
Kutokana na hali hiyo eneo la manzeze darajani miaka michache iliyopita kuliwekwa uzio kuanzia eneo la Agentina hadi Tip Top Manzese lilizunguushiwa uzio wa vyuma lengo likiwa kwa wale wanaotaka kuvuka karibu na eneo hilo kupita juu ya daraja.
Hakuna shaka uwekwaji wa uzio na watu wakitumia daraja kuvuka barabara hiyo ya morogoro ilisaidia kupunguza ajali katika eneo la Manzese ambapo kabla ya uzio huo ajali zilikuwa zikitokea na kupoteza maisha ya watu wengi na kuacha familia zikiwa yatima.
Baada ya uzio kuweka na kuchakaa na katika baadhi ya maeneo uzio huo umeanguka na watu kuanza kufanya njia ambayo kwa namna moja au nyingine ajali zinaanza kushamili tena katika eneo baada ya kipindi kirefu kupungua kutokana na uzio uliokuwepo awali.
Pia baadhi ya uzio ziligongwa na madereva wasiokuwa makini wanapokuwa barabarani na kusababisha upenyo kupatikana na watu kutumia upenyo huo kuvuka bila ya uangalifu na kusababisha kupata ajali na wakati upoteza maisha na viongo vyao na kuwaacha wakiwa na upungufu wa viongo vyao na kuanza kuwa tegemezi ilhali walikuwa wakifanya shughuli zao kabla ya kupata ajali.
Licha ya ajali kutokea katika eneo hilo baada ya uzio uliowekwa hapo kuzuia watu kupita na kutakiwa kutumia daraja baadhi ya uzio huo kugongwa na magari na na sehemu nyingine kuanguka kutokana na uchakavu wa vyuma hivyo hakuna jitihada zinazofanywa na mamlaka husika ili kutengeneza tena uzio huo.
Ukweli baada ya baadhi ya uzio huo kuanguka kutoka na sababu mbalimbali na zikiwemo zile nilizozieleza hapo awali, kuwepo kwa upenyo kwa baadhia ya maeneo kunasababisha watu kunyang’anywa mali zao wakati wa usiku na kufanyiwa vitendo vingine vichafu ambapo ni vyema sasa mamlaka husika ikachukua jukumu la kufanya matengenezo katika sehemu uzio umeanguka ili watu watumie daraja kuvuka barabara.
Pia watu wanaopita katika maeneo uzio uliopoangua ni vyema wakatumia busara na hekima kufikiria madhara yanaweza kupatikana baada kuvuka eneo hilo ambalo halina ishara za kivuko.
Ukubwa wa tatizo katika eneo hilo awali ulikuwa mkubwa ikizingatiwa eneo hilo linazungukwa na wafanyabishara wa mitumba kitu ambacho kinasababisha mkusanyiko mkubwa wa watu na endapo madereva wanaotumia barabara hiyo wasipokuwa makini ajali azitaweza kuhepukika katika eneo hilo .
Kibaya zaidi baadhi ya watu wasikouwa waaminifu wanakuwa wakichukua vyuma vilivyoanguka kutokana na kuchakaa au kugongwa na magari na kwenda kuviuza kama chuma chakavu.
Hakika si jambo jema kwa tabia hiyo ya watu wachache kuchukua vyuma hivyo na kwenda kuviuza na kujipataia fedha za kujikimu ambazo zinarudishs nyuma maendelea ya eneo, hivyo ni vyema raia wa eneo hillo wakawa walinzi kwa kitendo ambacho akistahili kuigwa na jamii yoyote inayo pendamaendeleo.
Pia kwa wale watakaofanikiwa kukamatwa baada ya kugonga uzio huo ni vyema jambo la kwanza wakapewa amri ya kutengeza uzio kabla ya hatua nyingine hazijafuatwa ili kuendelea kutunza kwa maslahi ya wanaotumia barabara hiyo ambayo kwa kuwepo uzio huo wataweza kutumia kivuko cha daraja na kupunguza ajali za mara kwa mara ambazo zinaweza kuhepukika kwa njia hiyo.
Wakati huo huo manispaa ya Kinondoni ambayo naamini ndyo yenye mamlaka ya kuungalia na kutunza uzio huo ni vyema wakawa wanafuatilia mara kwa mara na kutengeneza sehemu zilizoharibika ili kuhakikisha kunakuwa na usalama wa wapita njia ambao awajari usalama wao kwa kupita sehemu zilizowazi baada ya uzio kuanguka, kwa kugongwa na magari au kwa kuchakaa.




No comments:
Post a Comment