Wachezaji waelimishwe kuhusu mikataba yao
Na Hamisi Magendela
SIKU chache zilizopita wakati wa muda wa kuwasilisha maombi ya usajili na wengine kuhamishwa kwa mkopo kumalizika kwa malalamiko mengi kwa wachezaji.
Mengi ya malalamiko yalikuja baada ya sheria hiyo kuonekana mpya miongoni mwa wachezaji wengi na kila mmoja akihisi kuonewa.
Kutokana na hilo kila mmoja alikuwa akipigana kivyake kuhakikisha anataba haki yake ya msingi na wengine walikubali kwenda kwa mkopo kucheza katika timu nyingine kwa shingo upande.
Kibaya zaidi wachezaji wengi walikuwa wakilalamikia kutoshirikishwa katika hilo japo upande wa timu ukidai mchezaji hana uwezo wa kuhoji endapo atatakiwa kuhamishwa kwa mkopo.
Suala hilo ndilo lilikuwa likiwapasua vichwa wachezaji na kiungo Mwammedi Simba Banka akadai awezi kuwa kama kuku kununuliwa na kutojua wapi anapelekwa kuchinjwa au kufugwa.
Meshack Abeil kwa upande wake alisema ni vyema akaacha soka kuliko kutafutiwa timu ya kucheza bila ihali yake kwa maana yeye ndiye mwenye maamuzi ya kuchagua ni timu hipi anaweza kuitumikia na si kuchaguliwa na viongozi.
Baadhi ya viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) walidai kuwa taratibu za kuhamisha mchezaji ni lazima kuwe na mafiga matatu kwa maana ya mchezaji, viongozi wa timu anayotoka pamoja na timu anayopelekwa kwa mkopo wazungumze.
Pia wapo viongozi wa TFF awaliosikika wakisema kuwa mchezaji hana haki ya kuhoji wakati timu yake inapoamua kumpeleka kwa mkopo na kuletab mkanganyiko kila kukicha na kutojua lipi ni sahihi.
Na viongozi wa timu husika pia wakishikilia msimamo wao kuwa wako sahihi, pia hawakustahili kuwashilikisha wachezaji hao kwa kuwa wanabanwa na mikataba yao , hivyo hawapaswi kulalamika.
Baada ya vuta ni kuvute tukashuhudia wachezaji walioweka pingamizi la kupelekwa kwa mkopo wakivunja mkataba na kupewa stahili zao kwa roho safi na kuachana kwa mikono miwili na kila mmoja akichukua hamsini zake.
Hakika suala hilo bado linaleta mkanganyiko kwa wachezaji na wadau wa soka nchini na wakiendelea kuumiza vichwa lipi sahihi kati ya hayo yaliyokuwa yakisemwa na kuumizwa vichwa wadau wa soka nchini.
Yawezekana mkanganyiko huo unatokea kutokana na viongozi na wachezaji wengi kutojua sheria na taratibu za uhamisho wa mkopo kutoka timu moja kwenda nyingine.
Hivyo ni wakati sasa wa TFF kutoa semina elekezi kwa wadau hao wa soka ili kuondoa mkanganyiko huo ambao unayumbisha na kuleta migogoro isiyo ya msingi katika soka letu.
Naamini endapo kila mmoja akitambua nafasi yake kuanzia katika mikataba ya wachezaji hakutakuwa na matatizo suku za usoni kwa jambo lolote likalotokea baina yao .
Pia wachezaji wengi wanatakiwa kutojisahau katika suala zima la kujiendeleza kielimu kitu ambacho kitawafanya kutambua wa mambo mengi yaliyo kwenye mikataba yao na kuondoa migogoro isiyokuwa na msingi.
Wachezaji wengi wanakuwa na tabia ya kukacha kujiendeleza na elimu pindi wanaposajiliwa na timu kubwa kitu ambacho siyo sahihi kwao.
Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT) Kanali Mstaafu Idd Kipungu, ni miongoni mwa wadau wa soka wanaowapigia kilele kila siku wachezaji kujiendeleza kielimu na si kutosheka na timu wanazozitumikia.
Naamini Kipingu anaona mbali katika hili kwa maana mchezaji akiwa na elimu yake ya kutosha anaweza akafahamu mengi katika sula zima la sheria na taratibu za michezo.
Pia mchezaji mwenye elimu yake ya kutosha anaweza akafahamu kwa kiasi kikubwa juu ya mkatabwa wake na kuhusimamia ipasavyo.
Wachezaji wetu endapo wataendelea kuikimbia elimu wataendelea kuwa watumwa na kuendelea kulalamika kuwa wanaonewa, kumbe inawezekana walikosea wakatia ya kusaini mikataba hapo awali.
Na siku zote viongozi wa timu ni wajanja kupindukia katika kusainisha mikataba kwa wachezaji kwa kulinda maslahi yao na timu zao.
Hivyo wachezaji wanatakiwa kuwa makini bila ya kubabaika wakati wa kuingia mkataba ambayo siku za usoni zinakuja kuwaghalimu, kumbe matatizo yalianzia wakati wa kusaini mkataba.
Ni vyema endapo mchezaji hana elimu ya kutosha katika suala zima la mikataba ni bora akaghalimika kwa kutafuta mwanasheria wa kumsimamia zoezi hilo .
La kusisitiza hapo ni vyema wachezaji wetu wasikimbie elimu kwa maana hiyo ndiyo muuongozo wa michezom yao na mabo mengine kwa ujumla.




No comments:
Post a Comment