FIFA, CAF, TFF kuwanoa makocha nchini - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Thursday, October 20, 2011

FIFA, CAF, TFF kuwanoa makocha nchini

Na Asha Kigundula
MAFUNZO ya ukocha wa soka kwa ajili ya kupata leseni za daraja C kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) itafanyika ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuanzia Novemba 7 hadi 20 mwaka huu.

Ofisa Habari wa (TFF), Boniface Wambura, alisema kuwa makocha 30 wameteuliwa kushiriki mafunzo hayo.
Wambura alisema wakufunzi wanne, mmoja wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), wawili wa CAF na mmoja wa Chama cha Mpira wa Miguu Denmark (DBU).

Alisema mkufunzi wa FIFA atakuwa Jan Poulsen, kutoka CAF ni Sunday Kayuni (Tanzania), Kasimawo Laloko (Nigeria) wakati kutoka Denmark ni Kim Poulsen.

Makocha walioteuliwa kushiriki kozi hiyo ni Christopher Eliakim, Jumanne Ntambi, Kenneth Mkapa, Mussa Furutuni, Mecky Maxime, Gideon Kolongo, Maka Mwalwisi, Haji Amir, Tiba Mlesa, Stephen Matata, Wane Mkisi, Edward Hiza, Leonard Jima na Ahmed Mumba.

Wengine ni Peter Mhina, Absolom Mwakyonde, Maarufu Yassin, Mussa Kamtande, Wilfred Kidau, Eliasa Thabit, Dismas Haonga, Fulgence Novatus, Juma Mgunda, Hassan Banyai, Mohamed Tajdin, Sebastian Nkoma, Emmanuel Massawe, Gabriel Gunda, Abdul Nyumba na Richard Kabudi.

Pia, kutakuwa na kozi nyingine ya juu ya leseni za daraja B, ambayo inatarajia kufanyika baadaye mwezi Desemba mwaka huu.

No comments:

Post a Comment