Simba, Ruvu zaingiza mil 14/- Chamazi - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Thursday, October 20, 2011

Simba, Ruvu zaingiza mil 14/- Chamazi

Na Asha Kigundula
JUMLA ya sh milioni 14,755,000 zimeingia kutokana na mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya Simba na Ruvu Shooting iliyofanyika juzi kwenye Uwanja wa Azam uliopo Chamazi, Dar es Salaam.
Mchezo huo ulifanyika juzi ambapo Simba iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 na kuzidi kushikilia nafasi ya juu katika msimamo wa ligi hiyo.
Ofisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Boniface Wamburam alisema watazamaji waliokata tiketi kushuhudia mechi hiyo walikuwa 2,794.
Wambura alisema kiingilio kilikuwa sh. 5,000 kwa mzunguko na sh. 10,000 kwa VIP. Waliokata tiketi za VIP walikuwa 157.

Alisema baada ya kuondoa gharama za mchezo na Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ambayo ni sh. 4,180,763 kila timu ilipata sh. 3,172,271.19. Mgawo mwingine ulikwenda kwa uwanja (sh. 1,057,423.70), TFF (sh. 1,057,423.70), Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu- FDF (sh. 528,711.86), Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam- DRFA (sh. 422,969.49) na Baraza la Michezo la Taifa- BMT (sh. 105,742.37).

Wakati huo huo, Mdhamini wa Ligi Kuu ya Vodacom, kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom tayari imeshatoa hundi ya nauli kwa ajili ya klabu ambazo timu zake zinashiriki ligi hiyo. Mgawo uliotolewa ni kwa ajili ya mwezi Septemba na Oktoba.

Tayari klabu husika zimeanza kuchukua hundi zao kutoka TFF. Kwa mwezi Septemba kila klabu imepata sh. 4,732,142 wakati Oktoba ni sh. 5,622,321. Hivyo kwa miezi hiyo miwili kila klabu imepata sh. 10,354,463.

No comments:

Post a Comment