Wadau wa soka kutoa maoni TFF - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Thursday, October 20, 2011

Wadau wa soka kutoa maoni TFF

Na Asha Kigundula
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limesema lipo katika mchakato wa kutengeneza mpango wa maendeleo wa muda mrefu, wa kupata maoni kutoka kwa wadau wa mpira wa miguu nchini.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura, alisema nia ya TFF kufanyia kazi maoni ya wadau ni kwa ajili ya kuhakikisha yanaingia katika mpango huo.

Wambura alisema wadau wanakaribishwa kutuma maoni yao kupitia mtandano wa ambao ni tfftz@yahoo.com au sanduku la barua 1574 Dar es Salaam kwa ajili ya uboreshwaji wa soka nchini.
Ofisa huyo aliongeza pia kuwa maoni hayo yawe yametumwa hadi kufikia mwishoni mwa Novemba mwaka huu.

Pia, TFF kupitia Kurugenzi ya Ufundi itakutana na makundi mbalimbali kusikiliza maoni yao. Novemba 2 mwaka huu imepanga kukutana na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) na pia waandishi wa habari ambao nao watatoa maoni yao.

No comments:

Post a Comment