Na Asha Kigundula
MENEJA wa klabu ya Simba, Abdallah Kibadeni, ameondolewa katika benchi la ufundi na nafasi yake imechukuwa na aliyekuwa nahodha wa timu hiyo, Nico Nyagawa.
Chanzo chetu kutoka katika klabu hiyo kinasema kuwa Kibadeni aliondolewa katika benchi hilo mwanzoni mwa wiki hii.
Kimesema Kibadeni sasa atakuwa katika timu ya vijana chini ya miaka 20, ambao wanafanyia mazoezi yao kwenye Uwanja wa Kinesi, Dar es Salaam.
Chanzo hicho kiliendelea kusema kuwa kuwepo kwa Nyagawa katika benchi hilo ni baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyochukulia miezi miwili sasa kwa ajili ya kuanza kazi hiyo.
Jambo Leo iliamua kumtafuta Nyagawa kuzungumzia ili ambapo kiungo huyo wa zamani alisema ni kweli amejiunga katika kambi ya Simba jana baada ya kufikia makubaliano na viongozi wa Simba.
Alisema walikaa chini na kufanya mazungumzo ya mkataba mpya wa kuwa kwenye benchi hilo ambapo sasa imefikia muafaka na yuko tayari kuanza kibarua hicho.
"Tumekaa na viongozi na kukubaliana, ambapo sasa nipo kwenye kambi ya Simba kwa ajili ya kuanza kazi yangu kama ambavyo tumekubaliana," alisema Nyagawa.
Nyagawa aliyekuwa mchezaji wa timu hiyo, alikaa na uongozi wa klabu hiyo na kuamua kuvunja mkataba wa zamani kama mchezaji na kumpa mpya kama meneja wa klabu ya Simba.
Thursday, October 20, 2011
New
Nyagawa achukua mikoba ya Kibaden
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment