Squezer kumuanika bachela videoni - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Thursday, October 20, 2011

Squezer kumuanika bachela videoni

Na Hamisi Magendela
NYOTA wa muziki wa kizaki kipya nchini, George Kasela 'Squeezer' anatarajia kuachia video ya wimbo wake unaofanya vizuri katika vituo mbalimbili vya redio wa 'Bachelor' Novemba mwaka huu.
Akizungumza na Jambo Leo Dar es Salaa jana kwa njia ya simu akiwa Morogoro, Squeezer alisema anatarajia kufanya mazungumzo na Adam Juma wa visual Lab kwa ajili ya kazi hiyo.
"Tukifikia pazuri na Juma, video itafanyika mara moja na itakwenda hewani Novemba mwaka huu ili iende sambamba na Audio ambayo tayari nimeisambaza katika redio za mikoani na chache za Dar es Salaam," alisema Squeezer.
Nyota huyo wa kibao cha Nilikupenda, Squeezer, alisema huo ni ujio wake mpya na anashukuru kazi zake kukubalika kwa mashabiki wengi kitu kinachompa imani albamu inayofuata itafanya vizuri katika sanaa ya muziki wa kizazi kipya.
Amewaomba mashabiki kumpokea kwa mikono miwili kwa ujio wake huo, ambapo katika wimbo wa Bachelor ametoa hamasa kwa vijana wasiokuwa na ndoa kujitambua na kubadilika kwa ajili ya kujenga familia.
Alisema wimbo huo umetengenezwa katika studio ya Combination Sound, chini ya mtayashaji 'Man Walter' iliyopo mkoani mjini Morogoro.

No comments:

Post a Comment