Wambura sasa akimbilia Takukuru - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Monday, October 24, 2011

Wambura sasa akimbilia Takukuru

Na Asmah Mokiwa
MGOMBEA wa nafasi ya Uenyekiti katika Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mara (FAM), Michael Wambura amewasilisha suala la risiti na stakabadhi ya rufaa yake katika Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) ili kufanyia uchunguzi risiti hizo.
Hatua hiyo ni baada ya Wambura kuitwa katika kikao na Shirikisho la Mpira wa Miguu TFF kwa ajili ya ya rufaa iliyokatwa na Titus Osoro.
Alisema katika kikao hicho, mwanasheria wake, Audax alikataliwa kuingia  wakati kamati hiyo ikiwa na wanasheria wake wawili.
Alisema hatua hiyo pia imemfanya aandike rasmi malalamiko yake katika Chama cha Wanasheria cha Tanganyika  (Tanganyika Law Society) kulalamikia kwa nini wanasheria wao ambao pia ni wanachama wao wanazuia raia wasipate msaada wa kisheria na haki ya kutetewa na mawakili.
Wambura, alisema katika rufaa hiyo, mlalamikaji hakulipia ada ya rufaa kama kanuni na sheria za TFF zinavyotaka.
Alisema mpaka anafika katika kikao hicho, alikuwa hajaona rufaa hiyo, hivyo aliomba aione na kubaini kuwa haikuwa rufaa bali ni pingamizi, ambapo kipindi cha pingamizi kilishapita.
Alisema pingamizi hilo lilikuwa na risiti namba 0164 ya malipo, ambapo ilifanyiwa marekebisho na kufutwa tarehe 20 na isomeke 19 ili ionekane kuwa ni rufaa iliyokosa dosari.
Alisema baada ya kuwa na wasiwasi na stakabadhi hiyo aliweka pingamizi katika kikao hicho na kuwa kamati ya rufaa haikuwa na uwezo wa kusikiliza shauri hilo kwani haikuwa rufaa bali ni pingamizi.
Wambura, ambaye pia aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa kuchaguliwa wa Simba, alisema kupitia hilo, amebaini kuwa mlalamikaji alishirikiana na TFF katika suala zima la rufaa, kitu ambacho hakikuwa haki.

No comments:

Post a Comment