Na Hamisi Magendela
KAMATI ya mashindano ya ligi ya mchezo wa mpira wa Magongo yaliyosimama kwa ajili ya kupisha mashindano ya Afrika Mashariki ya kumbukumbu cha kifo cha Baba wa taifa Mwalimu Nyerere inatarajia kukaa Oktoba 28 kupanga tarehe ya kuanza mashindano hayo.
Akizungumza na Jambo Leo Katibu mkuu wa Chama Cha Mpira wa Magongo Mkoa wa Dar es Salaam (DRHA) Mnonda Magani, alisema ligi hiyo ilisimama ili kupisha mashindano hayo ambayo yalikuwa yakijumuisha baadhi ya timu za Dar es Salaam na mikoa mingine.
"Tulisimamisha kutoka na mashindano yale kujuisha na baadhi ya timu za Dar es Salaam ikiwemo Magereza, hivyo tutakaa Ijumaa na kujadili tarehe ya kuanza mashindano hayo", alisema Magani.
Ligi ya hiyo ya magongo inashirikisha timu tano za mkoa wa Dar es Salaam ambazo ni pamoja TPDF, Magereza Tanzania, Dar es Salaam Khalsa, DI, pamoja na Lugalo.
Timu ya TPDF inaongoza ligi hiyo ikiwa na pointi 10 ikifuatiwa na Magereza Tanzania nyenye point 9, hivyo Magani aliomba timu shiriki kufanya mazoezi ya kutosha ili kuleta upinza katika mashindanmo hayo yanayotarajia kuendelea katika viwanja vya Lugalo.
Tuesday, October 25, 2011
New
DRHA kujadili kuanza kwa ligi Oktoba 28
Subscribe to:
Post Comments (Atom)




No comments:
Post a Comment