Wambura ang'olewa uchaguzi Mara - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Tuesday, October 25, 2011

Wambura ang'olewa uchaguzi Mara

Na Asha Kigundula
KAMATI ya uchaguzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeondoa jina la mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti katika uchaguzi wa Mkoa wa Mara (FAM) Michael Wambura, baada ya kupeleka suala la mpira wa Miguu Mahakamani.
Akizungumza Dar es Salaam jana Mwenyekiti wa Kamati hiyo Deogratias Lyatto, alisema uhamuzi ulichukuliwa baada ya kudaiwa kukiuka katiba uanachama wa TFF kwa kupeleka shauri mahakamani la klabu ya Simba Mahakani.
Lyatto. alisema kwa mujibu wa katiba ya TFF Ibara ya 49 (1), katiba ya FAM ya Ibara ya 47 na kanuni zauchaguzi wa wanachama TFF Ibara ya 12 (1) Kamati ya Uchaguziya TFF ilifanya kikao Oktoba 23 na 23 mwaka huu kupitia mchakato wa uchaguzi wa FAM.
Alisema kamati ilipitia fomu za waombaji uongozi wote kujiridhisha kama katika ya FAM na TFF na Kanuni za uchaguzi za wanachama wa TFF zilizingatiwa pia na kujadili pingamizi Michael Wambura iliyowasilishwa na Titus Osoro.
Pia alisema kabla ya kikao hicho, kamati ya uchaguzi ya TFF katika kutekeleza wajibu wake wa kikatiba, iloituma wajumbe wawili kwenda kufanya kikao cha pamoja na kamati ya uchaguzi ya FAM Oktoba 5 mwaka huu.
Lyatto alisema katika hali ya kusikitisha usiku wa Oktoba 4 siku ambayo waliwasili mjini Musoma walipokea vitisho vya maandishi kutoka kwa waliojiita wadau wa soka wa mara na kutoa taarifa hiyo kwa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa wa Mara na kupokelewa na ofisa Tawala wa Mkoa (RAS).
Aliongeza kuwa baada ya kikao hicho cha Mara, baadhi ya wagombea walikaririwa na vyombo vya habari wakisema kuwa kamati ya uchaguzi ya TFF ilikwenda kuvuruga uchaguzi wa FAM, hivyo kamati inapenda kuwajulisha wadau wa mpira wa wa miguu hiyo ilifanya kazi kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi wa TFF
Hivyo kuwepo wajumbe wa kamati ya uchaguzi mkoani mara ni kwa mujibu wa katiba na si kwa utashi wao, kamati hiyo ingependa kuwajulisha wadau wa soka kuwa hii si mara ya kwanza kufanya hivyo.
Kwani iliwahi kufanya hivyo kwenye uchaguzi mkoani Rukwa, uchaguzi wa klabu ya Simba, Yanga , Villa Squad Coastal Union na mkoa wa Morogoro na kusiditiza kuwa hayo ni matakwa ya katiba ya TFF na si wanachamawake na Fifa ambazo zinataka kuwapo na kamati huru za uchaguzi.
Pia kamati hiyo ilisema kuwa taarifa zilizotolewa kupitia vyombo vya habari kuwa Mkoa wa Mara wanayo mabo yao wenyewe ya uendeshaji wa soka na hawapaswi kusimamimiwa na chombo chochote si za kweli na ni upotoshaji wa katiba ya FAM, Ibara ya 1(6) inatamka kama ifutavyo.
“ FAM ni mwanachama wa TFF, hivyo inawajibika kuheshimu katiba, Kanuni, Miongozo na Maamuzi ya TFF na kuhakikisha nayo yanaheshimiwa na wanachama wake”.

Lyatto alisema kamati hiyo imeridhika kuwa Magoti Magoti aliyeomba kugombea nafasi ya Mjumbe kamati ya Utendaji FAM hakutimiza masharti na kukosa sifa, ambapo kamati hiyo imeondoa jina lake katoka orodha ya wagombea.
Alisema maamuzi hayo yametolewa na kamati baada ya kuona wagombea hao hawana sifa na si kwa ajili ya pingamizi ambayo iliwekwa.
Lyatto alisema wao hawafanyi kazi kwa mamuzi ya mtu wao wanafanya kazi kwa mujibu wa katiba ya TFF, FIFA na FAM.

No comments:

Post a Comment