Na Mwandishi Wetu
MWAMUZI wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Oden Mbaga wa Dar es Salaam ndiye atakayechezesha mechi ya watani ya jadi kati ya Simba na Yanga, mchezo unaotarajiwa kufanyika Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari na Ofisa Uhisiano wa TFF, Boniface Wambura 'Bigbon', alisema kuwa mchezo huo namba 78 wa Ligi Kuu ya Vodacom yamekwenda vizuri katika kila idara.
Mara kadhaa, mwamuzi wa mechi hiyo anakuwa kwenye presha kubwa ya mshabiki wa pande hizo, hasa kutokana na tamaduni ama fikra ya kuubeba upande mmoja katika maamuzi, hivyo imepata kutokea kubadilishwa mwamuzi katika mazingira ya utata.
Waamuzi wasaidizi katika mechi hiyo ambao wote wanatambuliwa na FIFA ni Hamis Chang’walu wa Dar es Salaam ambaye atakuwa namba moja, na John Kanyenye (Mbeya) atakayekuwa namba mbili.
Mtathimini wa waamuzi (referee assessor) atakuwa Soud Abdi kutoka Arusha wakati kamishna wa mchezo huo ni Mohamed Nyange kutoka Dodoma.
Viingilio vya pambano hilo ni kama ifuatavyo, Viti vya kijani na bluu kiingilio kitakuwa sh. 5,000, viti vya rangi ya chungwa ni sh. 7,000, VIP C sh. 10,000, VIP B ni sh. 15,000 wakati VIP A itakuwa sh. 20,000.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepanga kuuza tiketi hizo siku moja kabla ya mchezo na siku yenyewe ya mechi katika maeneo ambayo yatatangazwa baadaye.
Wakati huohuo; Mechi namba 89 ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Kagera Sugar na Coastal Union iliyopangwa kufanyika Novemba 2 mwaka Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba imesogezwa mbele kwa siku moja.
Uamuzi wa kusogeza mechi hiyo hadi Novemba 3 mwaka huu umetokana na wamiliki wa Uwanja wa Kaitaba kuruhusu utumike kwa sherehe za Mwenge wa Uhuru.
Tuesday, October 25, 2011
New
Mbaga kumaliza ubishi Simba, Yanga
Subscribe to:
Post Comments (Atom)




No comments:
Post a Comment