NMB yashindwa kutamba Shirima Cup - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Tuesday, October 25, 2011

NMB yashindwa kutamba Shirima Cup

Na  Said Hauni, Lindi.
TIMU ya Soka ya NMB ya mjini hapa imeshindwa kutamba baada ya kukubali kipigo cha magoli 3-0 kutoka kwa Lindi Sports, katika mchezo wa kugombea kombe la kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi (Shirima Cup) uliofanyika jana uwanja wa Ilulu.
Lindi Sports ilianza kuhesabu bao la kuongoza katika dakika ya 36 ya mchezo lililowekwa wavuni na Ally Madilu,baada ya kupokea pasi ya Juma Athumani na kuujaza wavuni kwa kichwa.
Dakika 42 ya mchezo mchezaji Salum Selemani aliipatia goli la pili timu ya Lindi Sports kufuatia piga nikupige langoni mwa NMB na mfungaji kuuweka wavuni, hadi mapumziko Lindi ilitoka kifua mbele kwa ushindi wa mabao 2-0.
Kipindi cha pili kila timu ilirejea uwanjani ikiwa na nguvu mpya  baada ya kupewa mawaiza kutoka kwa makocha wao ambayo hata hivyo yalisaidia zaidi Lindi Sports.
 Alikuwa Salum Selemani tena aliipatia goli la tatu kitabu cha magoli, baada ya kufunga  dakika ya 76 ya mchezo baada ya kuwatoka walinzi wa timu ya NMB na kuwachia shuti kali lililotinga wavuni.

No comments:

Post a Comment