TBF yajiweka mikakati ya kimataifa - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Tuesday, October 25, 2011

TBF yajiweka mikakati ya kimataifa

Na Charity James
SHIRIKISHO la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF) limesema litahakikisha linaweka mikakati itakayowezesha mchezo huo kusonga mbele katika mashindano ya kitaifa na kimataifa.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Ufundi wa TBF  Jimmy Nkongo alisema kuwa ni jambo la msingi kuona mchezo huo unapewa kipaumbele ili kuuwezesha kupiga hatua kwa maslahi ya Taifa.
Alisema kupitia ligi ya mchezo huo ambayo imeanza kutumia vumbi  juzi jijini Dar es Salaam na kushirikisha timu kutoka Ilala, Temeke na Kinondoni itakuwa sehemu muhimu ya kuimarisha mchezo huo.
“Lengo letu shirikisho ni kuona tunapiga hatua zaidi katika mchezo wa kikapu ndani ya Afrika Mashariki, Afrika kwa ujumla ”alisisitiza.
Pia alisema shirikisho hilo lilikuwa linasimamia mashindano ya klabu bingwa kanda tano yaliyomalizika Oktoba 16, mwaka huu ambapo timu za Dar es Salaam zimeonesha uwezo mkubwa katika mchezo huo lakini akaongeza ni vema ukaendelea kuwa chachu.
Akifafanua zaidi kuhusu mashindani yaliyoanza juzi alisema kuwa ligi imeanza vizuri na itakuwa na msisimko wa hali ya juu hivyo ni vema timu shiriki zikaonesha umakini katika michezo yao.
"Timu zote zinazoshiriki katika ligi hii zimeweza kujiandaa vizuri .Tunaamini wachezaji wamepata mafunzo ya kutosha kutoka kwa walimu wao .Hivyo ni matarajio yetu kuona timu zikishindana kitaalamu,"alisema.
Pia limesema umefika wakati kwa timu zote zinazoshiriki mashindano ya mpira wa kikapu katika Mkoa wa Dar es Salaam kuonesha uwezo wao ili kufikia malengo.

No comments:

Post a Comment