Na Charity James
MWENYEKITI wa Baraza la Michezo Taifa (BMT) Dionis Malinzi anatarajia kuwadhamini wachezaji watakaoenda kushiriki mashindano ya Gofu ya wanawake nchini Uganda.
Katibu mkuu wa (TLGU) Anita Siwale alisema kuwa mwenyekiti huyo amehaidi kuwadhamini wachezaji wote watakaoenda katika mashindano hayo.
Siwale alisema bado haijajulikana ni wachezaji wangapi watashiliki mashindano hayo toka hapa nchini.
"Bado hatujajua tutapeleka wachezaji wangapi, lakini tutahakikisha wachezaji mara kwa mara wanapata nafasi ya kushiriki". Alisema Anita.
Katibu huyo alisema kuwa mbali na wachezaji hao hao pia watawapa nafasi wachezaji wote wa timu ya Taifa ya Gofu ya wanawake.
Mashindano hayo yanatarajiwa kufanyika Novemba mwishoni Nchini Uganda huku yakishilikisha Nchi za Afrika Mashariki.
Tuesday, October 25, 2011
New
Malinzi kuwadhamini wanashiriki Gofu Uganda
Subscribe to:
Post Comments (Atom)




No comments:
Post a Comment