Tambo za Matumla, Maneno homa tupu - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Monday, December 19, 2011

Tambo za Matumla, Maneno homa tupu

Na Mwandishi Wetu
TAMBO zinaendelea kwa mabondia Rashid Matumla ‘Snake Man’ na Maneno Osward ‘Mtambo wa Gongo’ wanaotarajia kupanda ulingoni kuzichapa Desemba 25 mwaka huu katika pambano lisilo la ubingwa.
Pambano hilo linatarajia kuwa la raundi 10 uzito wa kati litakalofanyika kwenye Ukumbi wa Heinken, Mtoni Kijichi jijini Dar es Salaam .

Siku kumi kabla ya mpambano, mabondia Rashidi Matumla na Maneno Osward walishauriana kupima vipimo mbalimbali vikiwemo Ukimwi na dawa za kuongeza nguvu kama wanatumia na walikamilisha zoezi hilo kwa daktari wa mchezo wa ngumi, Chales Kilaga.
Sheria za mchezo huo hazirusu kutumia dawa za aina yoyote ya kuongeza nguvu, hivyo mabondia wote wamekutwa wako fiti na wanatarajia kuzipiga Jumapili hii.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Adios Promotion, Shabani Adios 'Mwayamwaya', ambaye ndiye muandaaji wa pambano hilo, alisema limeandaaliwa ili kumaliza ubishi baina ya mabondia hao, ambapo katika pambano la mwisho, Matumla alimchapa Oswald kwa pointi na kuwalalamikia majaji kuwa hawakumtendea haki.
Na wameshawahi kupigana mara mbili nyuma, ambapo Matumla alimshinda Maneno mara mbili na Maneno kashinda mara moja, na mpambano huo utakuwa wa kumaliza ubishi baina yao.
Utasindikizwa na mabondia mkongwe Rashidi Ally atazichapa na Kulwa Mbuchi, Selemani Jumanne na Ibrahimu Madeusi wakati Shabani Zunga atavaana na Mohamedi Kashinde na bondia Sweet Kalulu na Saleh Mtalekwa
Katika mchezo huo, kutakua na DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokuwa zikisambazwa na kocha wa mchezo huo, Rajabu Mhamila 'Super D Boxing Coach' kwa ajili ya kuwapa mabondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki kujua sheria za masumbwi.
Super D, alisema katika DVD hizo kutakuwa na mapambano mengi ambayo yanaweza kutumika kama mafunzo muhimu kwa mabondia ,makocha marefa pamoja na mashabiki wa mchezo kujua sheria mbalimbali.
"DVD hizo ni nzuri na hata walio tayari tayari katika mchezo huo wanatakiwa kujua sheria na mafunzo ya ngumi mana zinafundisha mambo mengi,'' alisema Super D. DVD hizo za mafunzo zinapatikana makutano ya barabara ya Uhuru na Msimbazi au katika kambi ya ngumi ILala na klabu ya Ashanti iliyopo Ilala pia.

No comments:

Post a Comment