Mbunge wa Kigamboni, Dk. Faustine Ndungulile
Suleiman Msuya
SERIKALI imetoa sh. milioni 250 zimetolewa na Serikali kwa ajili ya ujenzi wa madarasa, mabweni, vyoo na maabara katika Shule ya Sekondari Nguva wilayani Kigamboni ili iweze kupokea wanafunzi wa kidato cha tano.
Hayo yamesemwa na Mbunge wa Kigamboni, Dk. Faustine Ndungulile leo jijini Dar es Salaam.
Alisema kupatikana kwa fedha hizo ni mwanzo mzuri wa kuifungua Kigamboni kielimu kwani kwa miaka mingi imekuwa haina shule ya sekondari ya kidato cha tano na sita.
“Sekondari ya Nguva iliyopo kata ya Somangila itaboreshwa na kuanza kutumika kama shule ya kidato cha tano na sita Serikali imetoa sh.milioni 250,” alisema.
Dk. Ndungulile alisema maboresho hayo yatakayoanza hivi karibuni yanatarajia kukamilika ifikapo mwezi Julai, mwaka huu.
Alisema kupatikana kwa shule ya kidato cha tano na sita, kutapanguza tatizo la wanafunzi waliofaulu kidato cha nne kwenda kusoma mbali.
Wednesday, March 15, 2017
New
SERIKALI YATOA MILIONI 250 UJENZI WA MADARASA KIGAMBONI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)




No comments:
Post a Comment