Suleiman
Msuya
WAKUU
wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Magereza Tanzania wametakiwa kuongeza
jitihada za uzalishaji na kuwasilisha taarifa ya utekelezaji kila miezi mitatu
kwa katibu mkuu wa wizara ya mambo ya ndani ya nchi.
Kauli
hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Manunuzi wa Wizara ya Mambo ya Ndani nchini,
David Mwangosi wakati akizungumza na makamanda wa shirika hilo jana katika
Ukumbi wa Bwalo Kuu la Maofisa Ukonga jijini Dar es Salaam.
Mwangosi
alisema shirika hilo linapaswa kuwa chachu ya uzalishaji wa mazao ili yaweze
kutosheleza wafungwa na jamii nyingine.
Alisema
iwapo kila kiongozi atasimamia majukumu yake na kuongeza uwajibikaji ni wazi
kuwa uzalishaji utaongezeka hivyo kutimiza matarajio ya Serikali ya kuifikisha
Tanzania ya viwanda na uchumi wa kati.
Mkurugenzi
huyo alisema kila viongozi ambao wanasimamia shirika hilo wanapaswa kuwa
wabunifu kwa kushawishi wadau mbalimbali ili kuweza kushirikiana katika miradi
mbalimbali.
“Nimekuja
hapa kumuwakilisha Katibu Mkuu, Meje Jenerali mstaafu Projestus Rwegasira na
amesema hataki mzaha katika kazi anataka kila baada ya miezi mitatu muwe
mnamletea taarifa ya shirika katika kuzalisha,” alisema.
Aidha,
mkurugenzi huyo amewataka makamanda wote ambao wanasimamia shirika na miradi
kuhakikisha kuwa wanaanzisha viwanda vidogo vidogo kwani ni chachu ya
maendeleo.
Mwangosi
alisema wizara ipo tayari kuunganisha Jeshi la Magereza Tanzania na nchi
mbalimbali ambazo zinaweza kusaidia uanzishaji wa viwanda vidogo.
Alisema
wizara ipo tayari kutoa mafunzo iwapo itahitajika hasa kwa wafungwa ambao
watakuwa wanatumiwa katika viwanda husika.
Kwa
upande mwingine mkurugenzi huyo wa manunuzi alisema wapo katika harakati za
kulipa madeni yote ambayo yamewasilishwa kwao ili kuondoa migogoro na wadai.
Alisema
pamoja na kuahidi kulipa madeni hayo pia aliwataka waandaaji wa taarifa
kuzingatia usahihi ili kuepuka kusumbuliwa mara kwa mara kutokana na
kutoeleweka.
Kwa
upande wake Kamishna Jenerali wa Magereza (CGP), Dk. Juma Malewa alisema jeshi
hilo lina miradi takribani 23 ya uzalishaji hivyo wanajipanga ili miradi hiyo
iwe na tija.
Alisema
shirika hilo linajihusisha na uzalishaji wa mahindi, maharage, mpunga, alizeti,
maziwa na nyama ambapo kutokana na changamoto mbalimbali yapo maeneo ambayo
hajafanya vizuri.
Dk.
Malewa alisema kutokana na uhaba wa fedha na kuchelewa kwa ruzuku uzalishaji wa
mbegu bora za kilimo umekuwa ukishuka
mwaka hadi mwaka
“Mhemiwa
mgeni rasmi shughuli za uzalishaji katika miradi ya viwanda vidogo vidogo
zimeendelea kufanya vizuri pamoja na changamoto za uchakavu wa mashine na
mitambo,” alisema.
Alisema
kutokana na maendeleo ya teknolojia viwanda vilivyopo vinahitaji mashine na
mitambo ya kisasa ili kukidhi uzalishaji wa bidhaa na ushindani katika soko.
Kamishna
Malewa alisema shirika linaendelea kutoa chakula kwa wafungwa ambapo hadi
kufikia Januari lilikuwa limefika zaidi y ash. bilioni 3.6 na deni kwa taasisi
za Serikali likifikia zaidi ya sh.
bilioni 3.
Dk.
Malewa alisema kwa sasa wanashirikiana na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa (NSSF)
na (PPF) kuendeleza shamba la miwa na Kiwanda cha Sukari Gereza la Mbigiri na
pia wanarajia kuendeleza s Shamba la Mbegu Bagamoyo lenye ekari 200.




No comments:
Post a Comment