Na Khadija Kalili
MKURUGENZI Mkuu, Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade)
Latifa
Khamis amesema kuwa kuwa kuanzia sasa serikali itafanya kazi na Chama
Cha Vipidozi Tanzania (TCA) ikiwa ni katika kuhakikisha wanalinda afya
za watumiaji wa vipodozi na sekta ya urembo na watanzania wote kwa
ujumla.
Mkurugenzi
huyo amesema hayo leo Desemba 10, 2022 wakati alipokuwa mgeni rasmi
katika uzinduzi Tamasha la siku moja 'Vipodozi Day' lililofanyika kwenye
viwanja vya Leaders Club Kinondoni Jijini Dar es Salaam ambapo
alimwakilisha Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji.
Amesema
enzi za kupenda na kithamini vipodozi au bidhaa kutoka nje ya nchi
zimepitwa na wakati. "Hivyo nachukua fursa hii kuwapongeza sana kwa
Tamasha hili la aina yake huku nikiwataka muongeze kasi katika
uzalishaji wa vipodozi visivyo na viambata vyenye sumu na nina waahidi
kuwa Tantrade tutawapa fursa ya kujitangaza kitaifa na kimataifa.
Nawakaribisha
TCA mtukimbilie muda wowote na milango iko wazi kwa ajili yenu huku
nikiwaahidi kuwa tutawatafutia masoko nje ya nchi kwani hii ni fursa
kubwa katika kuitangaza nchi kimataifa katika nyanja ya biashara pia
kuanzia mwakani tutawapa fursa ya kuonesha bidhaa zenu kwenye maonesho
ya Viwanda Tanzania pamoja na makongamano mbalimbali ya biashara kwa
kuwaunganisha na wadau mbalimbali kwa kupitia muamvuli wa TCA."
"Tasnia
hii ya vipodozi ina wigo mpana ambao umeongeza ajira na kukuza uchumi
kwa vijana na kinamama wa hapa nchi, Wanawake shikamaneni na mnyanyuane
kiuchumi ikiwa ni kwenye kuongeza kipato katika familia zenu. Amesema
Latifa Khamis
Kwa
Upande wa Mwenyekiti wa TCA, Shekha Nasser ameweka wazi kuwa inaonesha
kuwa wanawake wengi hasa wakaazi wa Wilaya ya Kinondoni ni wahanga wa
kunyonyoka kope kutokana na kubandika kope za bandia huku wakitumia
gundi ambazo zimewapatia madhara.
Pia
amewaasa wanawake kujenga Utamaduni wa kutumia vipodozi vya asili
visivyo na madhara huku akisema endapo watatumia mafuta ya mnyonyo
yanayoyengenezwa ni mwanachama wao Nzalakado yatasaidia kuziotesha kope
hizo. Bi Shekha ameiomba serikali iweze kuwapunguzi kodi kwenye bidhaa
za urembo ikiwemo saluni na kuwekwe muongozo ambao utakua ni rafiki
kwenye kulipa kodi kwa kupitia chama hicho TCA kilizinduliwa miaka
mitatu iliyopita Jijini Dar es Salaam ambao ni muunganiko wa wadau wenye
kuuza na kutengeneza vipodozi nchini.
Mkurugenzi Mkuu, Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade)
Latifa
Khamis akizungumza leo Desemba 10, 2022 alipokuwa mgeni rasmi katika
uzinduzi Tamasha la siku moja 'Vipodozi Day' lililofanyika kwenye
viwanja vya Leaders Club Kinondoni Jijini Dar es Salaam akimwakilisha
Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji.
Mwenyekiti
wa TCA na Mkurugenzi Mkuu Taasisi ya MANJANO FOUNDATION, Shekha Nasser
akizungumza leo Desemba 10, 2022 uzinduzi Tamasha la siku moja 'Vipodozi
Day' lililofanyika kwenye viwanja vya Leaders Club Kinondoni Jijini Dar
es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu, Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade)
Latifa
Khamis na Mkurugenzi Mkuu Taasisi ya MANJANO FOUNDATION, Shekha Nasser
pamoja na wageni waalikwa wakitembelea mabanda kujionea Tasnia ya
Vipodozi inchi inavyoendelea katika uzinduzi Tamasha la siku moja
'Vipodozi Day' lililofanyika kwenye viwanja vya Leaders Club Kinondoni
Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu, Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade)
Latifa
Khamis na Mkurugenzi Mkuu Taasisi ya MANJANO FOUNDATION, Shekha Nasser
pamoja na wageni waalikwa wakipata maelekezo walipotembelea mabanda
kujionea Tasnia ya Vipodozi inchi inavyoendelea katika uzinduzi Tamasha
la siku moja 'Vipodozi Day' lililofanyika kwenye viwanja vya Leaders
Club Kinondoni Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa katika uzinduzi Tamasha la siku moja 'Vipodozi Day' lililofanyika kwenye viwanja vya Leaders Club Kinondoni Jijini Dar es Salaam.
Picha ya Pamoja.Mkurugenzi
Mkuu, Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) Latifa
Khamis na Mkurugenzi Mkuu Taasisi ya MANJANO FOUNDATION, Shekha Nasser
pamoja na wageni waalikwa wakiwa katika Picha za pamoja katika uzinduzi
Tamasha la siku moja 'Vipodozi Day' lililofanyika kwenye viwanja vya
Leaders Club Kinondoni Jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment