TASAC YAKUTANISHA KAMPUNI ZA WAAGIZAJI WA MAFUTA YABAINISHA UMUHIMU WA UMOJA WA KUKABILI MAJANGA UMWAGIKAJI MAFUTA - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Sunday, December 18, 2022

TASAC YAKUTANISHA KAMPUNI ZA WAAGIZAJI WA MAFUTA YABAINISHA UMUHIMU WA UMOJA WA KUKABILI MAJANGA UMWAGIKAJI MAFUTA

 Habari kwa Hisani ya Chalila Kibuda wa Michuzi TV

SHIRIKA la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limekutana na Waagizaji wa Mafuta nchini  katika kujadili kuanzisha umoja wa kukabiliana na mwaafuta yanayomwagika katika Bahari kuwa nguvu ya pamoja ya kuweza kukabili pale umwagikaji wa mafuta.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TASAC Kaimu Abdi Mkeyenge , Meneja wa Usafiri wa Meli , Ulinzi na Mazingira Selestine Mkenda katika mkutano wa wadau wa Meli uliofanyika jijini Dar es Salaam amesema  kuwa mafuta yakimwagika katika bahari ni janga ambapo meli husika inatakiwa kulipa fidia kuhusiana na uchafuzi wa mazingira katika bahari.

Amesema kuwa uwepo wa umoja ni muhimu sana hasa kampuni za  uwagizaji  mafuta zisipokuwa na umoja ikitokea mafuta yamemwagika mafuta kwenye bahari fidia zikihitajika kampuni inaweza kufikisika.

Mkenda amesema kuwa waagizaji wa mafuta wakiwa na umoja wanaweza kununua  vifaa pamoja na kuwa na mfuko wa Rasilimali Fedha ya kuweza kukabili pale inapotokea mafuta yamemwagika katika bahari pamoja na maziwa.

Amesema kuwa mafuta yakimwagika kazi yao kama TASAC ni kusafisha eneo lililomwagika mafuta na baada ya hapo wanatafuta aliyesababisha.

Meneja huyo amesema mafuta yakimwagika yaliyosafishwa madhara yake sio makubwa kuliko mafuta ghafi mazito hivyo umoja huu ni muhimu kuwepo.

Mdau wa Uhifadhi wa Bahari na Maeneo Tengefu Claver Mwaikambo  amesema kuwa na majanga hayo yameshatokea ikiwemo nchini Kenya ambapo madhara yake yalikuwa makubwa.

Amesema kuwa waagizaji wa mafuta wakiwa na umoja utasaidia kukabili majanga pamoja na kufanya kampuni kuendelea kuwa imara kwenye kutoa huduma.

Mwaikambo amesema wakati umefika  kuwa na umoja kwani nyingi zina umoja zimeweza kukabili umwagikaji wa mafuta.

Mratibu wa Kupambana uchafuzi wa Bahari Zanzibar  Khalfan Hamad Hassan amesema kuwa vikao kukutanisha waagizaji wa mafuta ni muhimu katika kulinda mazingira.

Meneja wa Usafiri wa Meli , Ulinzi na Mazingira wa TASAC Selestine Mkenda akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mkutano wa TASAC na Waagizaji Mafuta juu kuanzisha umoja wa kukabiliana na umwagikaji mafuta kwenye bahari na maziwa , jijini Dar es Salaam.

 

Mdau wa Uhifadhi wa Bahari na Maeneo Tengefu Claver Mwaikambo akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na  athari ya mafuta yakimwagika katika bahari au ziiwa wakati wa mkutano wa TASAC na Waagizaji Mafuta juu kuanzisha umoja wa kukabiliana na umwagikaji mafuta kwenye bahari na maziwa , jijini Dar es Salaam.
Mdau wa Uhifadhi wa Bahari na Maeneo Tengefu Claver Mwaikambo akitoa mada ya athari ya mafuta kwenye mkutano wa TASAC na Waagizaji Mafuta juu kuanzisha umoja wa kukabiliana na umwagikaji mafuta kwenye bahari na maziwa , jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa Kupambana uchafuzi wa Bahari Zanzibar  Khalfan Hamad Hassan akizungumza na waandishi wa habari juu umhimu wa uanzishwaji wa umoja wa kukabiliana na umwagikaji wa mafuta kwenye bahari au ziwa , jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment