NA MWANDISH WETU
Shule za Serikali zimeshauriwa kuanzisha utaratibu wa utoaji wa motisha kwa walimu wanaofaulisha vizuri watahiniwa ili kuwapa moyo wa kufundisha kwa bidii.
Makamu Mwenyekiti wa kamati wa kamati ya kudumu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya elimu,utamaduni na Michezo, Husna Sekiboko alitoa ushauri huo jana wakati wa mahafali ya 21 ya kidato cha sita ya shule ya wasichana ya ST Christina ya jijini Tanga.
Akizungumza baada ya kushuhudia walimu wa shule hiyo ambao masomo yao watahiniwa wa kidato cha nne wamepata alama A na B Sekiboko ambaye pia ni Mbunge wa viti maalumu CCM Mkoa wa Tanga alisema motisha inawasukuma walimu kufundisha kwa juhudi zaidi.
"Nimeshuhudia hapa walimu wakipokea sh 5.milioni wengine 4.milioni kulingana na idadi ya wanafunzi katika somo lake waliofaulumu mtihani wa kitaifa wa kidato cha nne... nimejifunza kwamba hata shule za Serikali tunahitaji kuiga japo si kwa kiasi kama hiki lakini ifananie na kazi aliyofanya mwalimu" alisema Sekiboko.
Makamu huyo Mwenyekiti wa kamati ya Bunge alisema kulingana Serikali inapopata fedha inatakiwa kuajiri walimu wengi ili kuweka uwiano na idadi ya wanafunzi madarasani.
"Serikali kwa kadiri inapopata fedha ni vyema ikatupia jicho katika kuajiri walimu wengi zaidi ili kuweka uwiano na idadi kubwa ya wanafunzi kwenye shule za Serikali" alisema Sekiboko.
Mkuu wa shule hiyo,Hilda Kaniki alisema uongozi umeweka utaratibu wa kumzawadia sh 70 mwalimu sh 70,000 kwa kila mwanafunzi anayefaulu kwa alama A katika somo lake, na alama B sh 50,000 na kwamba hakuna motisha yoyote kwa alama C.
"Kwa hivyo ukizidisha kwa idadi ya wanafunzi waliopata alama A au B unakuta mwalimu mmoja anaibuka na sh 5.milioni.kama mlivyoshuhudia walipokabidhiwa" alisema Hilda.
Katika maonesho yaliyofanyika kwenye maabara ya shule hiyo,wanafunzi wa kidato cha tano waliweza kufanikiwa kumpasua nankisha kumpandikiza figo sungura aliyekuwa hana figo na akaweza kuendelea kuishi.
Katika risala iliyosomwa na Kelly Elvis kwa niaba yavwahitimu wa kidato cha sita alisema jumla ya wanafunzi 140 wanatarajiwa kufanya mtihani wa taifa wa kuhitimu huku shule hiyo iliyoanzishwa mwaka 2001 ikiwa na idadi ya wanafunzi 518 wanaochukua masomo ya sayansi,Sanaa na lugha za kifaransa kichina na kiingereza.
No comments:
Post a Comment