SHIRIKA la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limetekeleza dhana ya ukuaji wa uchumi kidigitali Kwa kuzindua akaunti ya kidigitali ya kuweka na kutoa fedha ijulikanayo kama akaunti pepe Kwa kutumia simu janja ya mkononi.
Kwa kutumia akaunti hiyo haimlazimishi mteja kuwa na Kadi ya
benki badala yake atatumia simu ya mkononi.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Biashara Tanzania (Tantrade) Latifa
Khamis amezindua akaunti hiyo july 9 iliyobuniwa na TTCL katika Maonesho ya 47
ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba yanayoendelea Dar es Salaam
amesema Kwa kutumia akaunti hiyo mteja alazimiki kuwa na akaunti ya benki
badala yake anapaswa kuwa na simu janja pekee.
Amesema ubunifu uliofanywa na TTCL ni wa kipekee kwa kufungua
akaunti inayotumika na simu janja ya mkononi ,huduma ambayo imekuja kwa wakati
muafaka wa matumizi ya kidigitali.
“Ni huduma iliyokuja
wakati muafaka,ikirahisisha upokeaji wa fedha,ikichochea biashara mdogondogo na
kubwa,” amesema Latifa na kuongeza kuwa ni mfumo unaosaidi kutotmbea na
fedha (cashless) na kuongeza usalama wa fedha pia.
Amesema akaunti hiyo inatumiwa na wateja wote wa mitandao ya
simu za mkononi ambapo inafungua fursa zaidi Kwa wananchi.
Amesema TTCL imeleta mapinduzi makubwa kwa sekta hiyo
ikirahisisha wasiokuwa na akaunti katika benki kuweza kutumia mfumo huo na
kunufaika na usalama wa fedha.
” Ni mfumo wenye
kuchochea uchumi na kukuza sekta ya fedha lakini pia inachochea uwekezaji,” amesema Latifa.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa T-Pesa,Lulu Mkude amesema uzinduzi
wa akaunti hiyo ni wa kipekee wenye na kuleta maendeleo makubwa ya teknolojia
ambapo inatoa fursa kushiriki uchumi wa kidigitali.
Amesema itachochea maendeleo ya uchumi ambapo inatumika
kupokea,kutumia fedha, kulipa bima mbalimbali na manunuzi ya kidigitali ambapo
pia ni ya Kila mmoja.
Amesema mteja anaweza kujiunga na kufurahia huduma za kifedha za
kidigitali na kinachotakuwa mteja kuwa na simu janja ya mkononi na kupakua
mfumo huo kupitia simu yake kupitia T-Pesa App na kufuata mtiririko kisha akaunti
hiyo kufunguliwa.
Amesema ni akaunti ya kurahisisha huduma za kifedha ambayo ni
hatua muhimu katika kukuza huduma za fedha.







No comments:
Post a Comment