Mhandisi Mtaalam wa Uchenjuaji Madini wa
Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Mhandisi Happy Mbenyange, kizungumza na
mwananchi aliyefika katika Banda la Taasisi hiyo kujionea shughuli mbalimbali
zinazofanywa na Shirika hilo kwenye Maonesho ya sabasaba Jijini Dar es Salaam.MKURUGENZI Mtendaji wa Shririka la Madini la Taifa (STAMICO), Dkt. Venance Mwasse amesema kuwa Bidhaa yao ya mkaa mbadala (Rafiki Briquettes) tayari imeingia kwenye mkakati wa Taifa wa nishati safi ya kupikia, na kwamba ifikapo mwaka 2033 kila mtu anatakiwa aachane na matumizi ya mkaa wa miti na kuni.
Dkt. Mwasse amebainisha hayo hivi karibuni alipozungumza na
waandishi wa habari kwenye maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba)
yanayoendelea Jijini Dar es Salaam.
Amesema kuwa Serikali ya Tanzania inayoongozwa na Rais Dkt.
Samia Suluhu Hassan imekuwa mstari wa mbele kuhamasisha wananchi juu ya
utunzaji mazingira kwa kutumia nishati safi ya kupikia, na kwamba ifikapo mwaka
wa 2024 Taasisi zote zinatakiwa ziachane na matumizi ya mkaa wa miti pamoja na
kuni.
“Tumefanya utafiti kwa
miaka mitatu kwa kuzihusisha taasisi zetu za utafiti ikiwemo COSTECH, Vyuo
Vikuu, na TIRDO. Sambamba na hilo, pia tumefanya uzalishaji pale TIRDO ambao
ulifanikiwa kwa kiasi kikubwa, hatukuishia hapo tukawaalika na wenzetu wa
Viwango TBS, ambao walienda kuuchunguza na mwisho wa siku tumepata cheti cha
TBS kwamba Bidhaa hii sasa imekidhi viwango kwa matumizi ya Binadamu” amesema Dkt.
Mwasse.
Ameongeza kuwa katika Maonesho ya Sabasaba mwaka huu STAMICO
imeendelea kutoa elimu kwa wanachi juu ya umuhimu wa matumizi ya nishati safi
ya kupikia ikiwemo mkaa huo, na kamba hivi karibuni Bidhaa hiyo itaanza
kupatika katika mikoa mbalimbali Bara na Visiwani.
“Tupo kwenye maonesho
hayo kwaajili ya kuonesha Biashara zetu na shuguli tunazozifanya, kama
mnavyoona tumekuja hapa kuwaonesha watanzania bidhaa tulizo nazo ikiwemo mkaa
mbadala (Rafiki Briquettes) na tumelitolea wasilisho maalum ili kila mmoja awe
na uelewa”
“Wito wangu, watanzania
waelewe kwamba sasa hivi tunakwenda kwenye Dira mpya na sera ya nishati safi za
kupikia ambayo inaelekeza kuachana na matuimizi ya mkaa wa miti au kuni, na
kuhakikisha kwamba tunatunza mazingira yeu. Tujiepushe na ukataji miti, hii
itapelekea kuachana kabisa na changamoto za Mabadiliko ya tabia nchi” Ameongeza.
STAMICO ni Shirika la Serikali chini ya Wizara ya Madini ambalo
lilianzishwa kwa sheria ya Mashirika ya Umma sura 257 kupitia agizo la
Uanzishwaji wa Shirika la Madini la Taifa namba 163, mwaka 1972 na kufanyiwa
marekebisho mwaka 2014.
CR- GREEN WAVE MEDIA







No comments:
Post a Comment