Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba akisaini kitabu cha wageni katika banda la Wizara ya Fedha kwenye Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, yanayoendelea katika viwanja vya sabasaba, Barabara ya Kilwa, jijini humo. Kulia ni Katibu Muhtasi wa Wizara hiyo, Bi. Masia Msuya.
NA FARIDA RAMADHANI, WF – DAR ES SALAAM
KATIBU Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba amewataka wananchi kuendelea kuiamini Serikali kwa kuwa mambo yote iliyoyapanga yatatekelezwa kikamilifu.
Ametoa
rai hiyo alipotembelea na kuzungumza na washiriki wa banda la Wizara ya Fedha
katika Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, yanayoendelea
katika viwanja vya sabasaba, Barabara ya Kilwa, jijini humo.
Dkt.
Mwamba alisema katika kipindi hiki cha utekelezaji wa Bajeti Kuu ya Serikali
iliyosomwa hivi karibuni, Serikali itahakikisha inatekelezwa kiufasaha na
kufukia malengo yaliyo kusudiwa.
Akizungumzia
Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, yanayoendelea katika
viwanja vya sabasaba jijini humo, aliwahamasisha wananchi wajitokeze kwa wingi
ili kupata elimu kuhusu masuala mbalimbali ya biashara na uwekezaji.
“Hapa
ni kwa ajili ya biashara, viwanda na uwekezaji, kuna mengi ya kujifunza ambayo
yatawezesha wananchi kujiinua kiuchumi”, alibainisha Dkt. Mwamba.
Alisema
katika banda la Wizara ya Fedha, washiriki wanaari ya kuwahudumia wananchi
hivyo watakapo tembelea maonesho hayo wasisite kupitia banda hilo muhimu katika
kusimamia uchumi wa nchi.
“Washiriki
wamejipanga na kwa namna wanavyotoa elimu ni rahisi mno kuwaelewa na kufanya
maamuzi sahihi kutokana na elimu iliyopatikana” alifafanua Dkt. Mwamba.
Aidha,
alionesha kufurahishwa na namna ambavyo wananchi wameonesha kufurahishwa na
kuondolewa kwa tozo za miamala ya simu na kubainisha kuwa lengo la Serikali ni
kuhakikisha inapunguza maumivu kwa wananchi.





No comments:
Post a Comment