MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kinondoni, Shaweji Mkumbura . ameitaka jumuiya ya Umoja wa Wanawake (UWT) Kinondoni, kuanza mapema maandalizi ya chaguzi mbalimbali ikiwemo wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu kwa lengo la kupata ushindi wa kishindo.
Pia, alimshukuru Rais Dk. Samia kwa kutoa fedha za utekelezaji
wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika Wilaya hiyo jambo ambalo limesababisha
kuleta mabadiliko makubwa.
Mwenyekiti Mkumbura aliyasema hayo jijini Dar es Salaam jana na
wakati akifungua mkutano wa Baraza la Umoja huo Wilayanjni humo uliohusisha
wajumbe na viongozi mbalimbali.
“Hakuna muda mrefu
wakujipanga kuingia katika chaguzi mbalimbali, hivyo katika mambo yenu ikiwemo
vikao, ajenda moja wapo iwe maandalizi ya Uchaguzi.
“Watu wengi wanaiangalia
na kuipigia mahesabu Wilaya yetu, hivyo wasipo fanya jiandaa mapema tunaweza
tusifanye vizuri, kwahiyo wakati ndio sasa wakujiandaa, “ alisisitiza
Aliwataka kufanya jitihada za kuongeza idadi ya wanachama
kutokana na idadi kubwa ya watu walioko katika Wilaya hiyo, hivyo waweke
mkakati mkubwa wa kuongeza wanachama.
“Tujipange tuache kukaa
tu nyumbani, maofisini, bali tuzunguke kutafuta wanachama. Hakuna sababu ya
kukaa maofisini, tufanye ziara za mara kwa mara kwenda kuwahamasisha wananchi,” alisema
Pia, alisisitiza uanzishaji wa miradi ya jumuiya kwani ni
mikubwa, kuondoa hali ya utegemezi hivyo Wilaya hiyo inatakiwa kuwa mfano wa
kuigwa kwa wengine.
Aliwataka kuwa na nidhamu na kuheshimiana kwani hata Chama
kimejengwa chini ya misingi ya nidhamu zaidi, hivyo kila mmoja anatakiwa
kutekeleza hilo.
Aidha, amewataka kuendelea kutekeleza jukumu lao la kuongeza
wanachama ikiwa ni sehemu ya kuimarisha uhai wa Jumuiya hiyo Wilayani humo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa UWT Wilaya hiyo, Anna Joseph
alisema, wanaendelea kumuunga mkono Rais Dk.Samia katika kutekeleza miradi
mbalimbali ya maendeleo.
Alisema kutokana na kazi kubwa iliyofanywa na Rais Dk. Samia
kazi yao kubwa ni kumpatia kura za kishindo mwaka 2025.
Kwa upande wake Katibu wa Umoja huo, Aziat Salim, alisema
wanayomipango mbalimbali ya kkujiimarisha kiuchumi kwani hadi sasa wanavyo
viwanja sita ambavyo wanakusudia kujenga miradi mbalimbali.






No comments:
Post a Comment