NA JOHN MARWA
NI hatareee, ndivyo unaweza kuelezea mara baada ya Klabu ya Simba
kutangaza mchana wa leo kuwa uzinduzi wa jezi yao ya msimu ujao watautambulisha
juu ya kilele cha Mlima Kilimanjaro.
Hayo yamesemwa leo na Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo Imani Kajula, amesema
wanaenda kuzindua jezi kwa njia tofauti ambayo haijawahi kutokea.
"Tutaenda kuzindua
jezi zetu katika njia tofauti. Sisi tunafanya vitu tofauti, haijawahi kutokea.
"Nawaambia rasmi hapa kwamba jezi ya Simba itazinduliwa juu ya
Mlima Kilimanjaro. Itaanza kupandishwa siku ya jumatano na watakuwa kileleni
siku ya ijumaa na juma mosi jezi itakuwa kwenye maduka yote nchini.
"Ijumaa saa 1:00 usiku jezi itakuwa imefika kileleni kwenye Mlima
Kilimanjaro. Itazinduliwa na kuonekana siku hiyo"amesema Kajula.
Kwa kufanya hivyo Simba itakuwa klabu ya kwanza kufanya hivyo na itabaki
kuwa historia nzuri kwa klabu hiyo ambayo ni klabu bora Ukanda wa Afrika
Mashariki na Kati ikishika nafasi ya Saba Barani Afrika.





No comments:
Post a Comment