MAENDELEO BANK YAJIVUNIA MAFANIKIO KWA MWAKA WA FEDHA WA 2022 NA YATANGAZA GAWIO KWA WANAHISA WAKE LA SH. MIL.708 - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Wednesday, August 9, 2023

MAENDELEO BANK YAJIVUNIA MAFANIKIO KWA MWAKA WA FEDHA WA 2022 NA YATANGAZA GAWIO KWA WANAHISA WAKE LA SH. MIL.708


Mkuu wa Idara ya Usimamizi, Athari na taratibu za Benki, Peter Tarimo (katikati) akitoa taarifa za mafanikio ya benki hiyo kwa mwaka wa fedha wa 2022 na kutangaza gawio kwa wanahisa wao, mchakato utakaofanyika Oktoba 6 mwaka huu.

NA MAGENDELA HAMISI

MAENDELEO BANK imetangaza gawio kwa wanahisa la Tsh. Mil 708 kwa mwaka wa fedha wa 2022 huku ikiongezeka kwa asilimia 136 tofauti na gawio la mwaka 2011 ambalo lilikuwa sh. mil 11.

Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es Salaam na Mkuu Idara ya Usimamizi wa Athari na Taratibu za Benki, Peter Tarimo na kufafanua kuwa baada ya kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa tisa wa wanahisa wamepitisha kwa pamoja mapendekezo ya Bodi ya Wakurugenzi kwa gawio la sh. mil 26 kwa kila hisa na kufanya jumla kufikia gawio la mil 708.

“Napenda kuchukua nafasi hii kuwafahamisha wanahisa wote kwamba gawio lao litalipwa Oktoba 6 mwaka huu kwa wanahisa wote ambao wamo regista ya wanahisa kwa tarehe 31Augusti 2023,” amesema.

Ameongeza kuwa ni wanne na wa pili kwa pesa taslimu tangu kuanzishwa benki hiyo mwaka 2013 na inaonyesha dhamira yao ya kuwatunza wanahisa  kwa umiliki wao.

Amesema kuwa wanajisikia fahari kupiga hatua kimafanikio tofauti na mwaka 2022 kwa kutekeleza adhima ya kuwahudumia wateja wao kalingana na wanajipanga na kujiwekea mikakati imara katika kufanikisha malengo.

Anaweka wazi kuwa hali hiyo ya kupiga hatua inawapa moyo na kuwaongezea ufanishi katika mikakati yao mbalimbali ya shughuli za kijamii inayofanikisha kujiendesha kwa faida.

“Benki ilipata faida kabla ya kodi y ash. Mil 1,984 kwa mwaka ulioishia desemba 31 mwaka 2022 (2021: TZS milioni 706 ) na mapato baada ya kodi yalikuwa sh. mil. 1,416 ikiwa ni ukuaji wa 141% ikilinganishwa na sh. mil. Tsh 587 mwa”ka 2021.

“Katika mwaka huo juhudi kubwa zilifanywa ambapo faida ya benki iliongezeka kwa sababu ya kutafuta njia mpya za biashara na kuendelea kutoa huduma za kiushindani,” amesema.

Tarimo, amefafanua kuwa juhudi za uwekezaji zilizofanywa katika mwaka huo zilisababisha ongezeko la 31% katika viwango vya riba. Mapato halisi ya riba yalikua mwaka hadi mwaka hadi kufikia sh. mil. 9,911 kutoka sh. mil. 7,538 mwaka 2021.

Amesema ongezeko la mapato ya riba halisi ni matokeo ya ongezeko la mikopo la sh. mil. 2, 942 kutoka baki ya mikopo ya sh. 57,716 mwaka 2021 hadi Tsh. mil. 60, 658 mwaka 2022  na riba ya uwekezaji katika dhamana iliongezeka kwa sh. 1,667 kutoka sh. 2,089 mwaka 2021 hadi sh. mil. 3,756 mwaka 2022.

Baada ya mafanikio, Tarimo amesema malengo yao ya kimkakati ni kuwa benki ya kitaifa itakayokuwa na matawi katika mikoa mbalimbali ya Tanzania na wanaamini kwamba watafikia adhima hiyo katika kipindi cha miaka mitano ya mpango mkakati cha mwaka 2022 hadi 2026.

Naye Meneja wa Usajili Hisa na Hati Fungani, Gideon Kapange ametoa wito kwa wanahisa wote ili wafanikishe mchakato wa kuchukua fedha wanatakiwa kupeleka taarifa zao mapema na ili kupata taarifa kamili wanapatikana kwa simu 0746140516.

“Hadi sasa wapo baadhi ya wanahisa ambao hatuna taarifa zao kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo wakati walipokuwa wakijisalijili hawakuwa wamekamilisha taarifa zao.

Pia wapo wengine kutokana na akaunti kutotumika mara kwa mara zimefungwa hivyo wanatakiwa waje ili wahakiki na wakamilishe taratibu zinatakiwa,” amasema.

No comments:

Post a Comment