

.........................................................
CHAMA cha Watu Wenye Ualbino
Tanzania (TAS) na Kituo Cha Sheria na Haki za Binadamu, wamelaani kitendo
kilichofanywa katika kilele cha siku ya simba Day 6 / 8 /2023 kufatia tukio la
kumtumia mtu mwenye ualbino akiwa katika hali ya nusu utupu ( kuvalishwa nepi)mbele
ya maelfu ya mashabiki katika uwanja wa taifa.
Akisoma tamko hilo jijini Dar es salaam
Mwenyekiti wa taifa wa chama cha watu wenye ualbino, Godson Mollel amesema
vitendo hivi vinatweza itu wa watu wenye ualbino nchini pamoja na kukiuka
katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ibara ya 12(2).
"Tunalaani tukio hili pamoja na matukio
mengine ambalo lilishafanywa na timu hiyo pia mwaka jana 8/ 8 / 2022 siku ya
simba day kwa kutumia jeneza na msalaba pamoja na kimnasibu mtu mwenye ualbimo
kama msukule" Alisema Bw. mollel.
Alisema vitendo hivi pamoja na kuwa vinautweza
utu wa watu wenye ualbino pia vimekuwa vikizua mijadala hususani katika jamii
na mitandaoni kufatia kuonyesha dhihaka kwa watu wenye ualbino kinyume na haki
za binadamu.
Bw mollel aliongeza kuwa pamoja na jitihada za
miaka mingi za utetezi wa watu wenye ualbino nchini katokana na historia ya
madhila wanayopitia jambo ambalo limekuwa likipelekea kusababisha idadi kubwa
ya wahanga wa vitendo vya ukatili na unyanyapaa.
"Kwa mda mrefu katika jamii nyingi watu
wenye ualbino wamekuwa wakihusishwa na mila na tamaduni mbaya zinazotweza utu
wao hivyo kushamili kwa vitendo hivi ni kuendelea kudidimiza juhudi za
serikali, mashirika watetezi na wadau binafsi za kueleimisha jamii kuhusu
ualbino" Alisema Bw Mollel
Kwa upande wake mkurugenzi wa LHRC, Wakili
Anna Henda amesema wanatambua utani wa jadi kati ya timu hizo mbili Simba na
Yanga bado sio jambo la kuhalalisha vitebdo vya kutweza utu wa mtu kwa sababu
yeyote ile iwe kwa kukusudia ama kwakutokukusudia.
Alisema vitendo vya namna hii vinaporuhusiwa
kufanywa hususani na taasisi kubwa na yenye ushawishi katika jamii kama timu ya
Simba zinarudhisha nyuma jitihada zote zinazochukuliwa kukuza na kuhanasisha
taswira chanya.
"Tunalaani kitendo hiki pamoja na vitendo
vyote ambavyo vinakiuka na kutweza utu kwani vitendo vya namna hii
vinapofabyika tena mbele ya hadhara mbele ya maelfu ya wananchi na kufatiliwa
duniani kote ni kurudisha nyuma jitihada zote za kukuza na kuhamasisha
taswira chanya ya watu wenye ualbino mbele ya jamii" Alisema wakili Henga.
Aidha wakili Henga ametoa rai kwa taasisi zote
hususani zenye ushawishi katika jamii kuepukana na vitendo hivi na kujikita
zaidi katika kuhamasisha heshima na utu hususani kwa watu wenye ualbino nchini.
CR HARAKATI ZA JIJI BLG
No comments:
Post a Comment