MJEMA: NENDENI MKANENE MAZURI AMBAYO YAMEFANYWA NA CCM - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Wednesday, August 23, 2023

MJEMA: NENDENI MKANENE MAZURI AMBAYO YAMEFANYWA NA CCM



NA MWANDISHI WETU

VIONGOZI wa Jumuia ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) wametakiwa kuzungumza mazuri ambayo yamefanya na chama na Serikali ili kiendelee kushika hatamu za uongozi wa taifa na shughuli zote za umma kwa maslahi ya watanzania.

"CCM inasema na inatekeleza kwa vitendo na hakuna jambo ambalo limesimama na hilo linatokana na ukubwa wa chama chetu barani Afrika na Dunia kwa ujumla, kwa kusimamia mifumo na demokrasia hali inayopaswa kwa viongozi wa jumuia zote kuwa na uelewa wa pamoja kuhusu kazi, misingi na majukumu ya kiutendaji.

Pia kiongozi hawezi kupanda jukwaani bila kuelewa taratibu na misingi ya chama inayotokana na vikao, jambo litakalosaidia kuchambua hoja kwa ufanisi na kuitetea CCM katika majukwaa ya kisiasa.

Hayo ameyasema leo Agosti 23,2023 na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Sophia Mjema, wakati akifungua mafunzo ya Itikadi na falsafa kwa viongozi wa Jumuia za chama hicho jijini Dar es Salaam waliochaguliwa kushika nyadhifa  mbalimbali katika uchaguzi wa mwaka 2020.

“Katika kikao kilichoongozwa na Rais wetu, Mama Samia Suruhu Hassan ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama chetu, kilifanyika miezia kadhaa iliyopita alitoa maagizo kuwa itolewa elimu kwa wanachama wetu ya  Ilani na Itikadi ili wafahamu mwenendo, maelekezo na muelekeo wa chama jambo litakalofanya kuwa na kauli moja kwa viongozi wote,” amesema.

Pia amesema katika ziara mbalimbali ambazo wamefanya wamepata majibu kuwa wapo baadhi ya viongozi wenye uelewa mdogo kuhusu Ilani na Itikadi ya chama, wengine hawafamu kabisa na kusababisha kutolewa kwa maagizo hayo.

Aliongeza kuwa anaamini baada ya mafunzo hayo, viongozi wa chama na jumuia zake watakuwa na uelewa wa pamoja juu ya kazi zao, majukumu ya kiuongozi na kufahamu vizuri misingi ya chama katika mfumo wa vyama vingi.

“Mtakapopata nafasi ya kuongea kwenye majukwaa, hutakiwa kuongea kama wewe, hiki chama si cha chako bali ni cha wanaccm, hivyo unaposisimama na kuongea fikiria maslahi ya chama kwanza kwani unaongea kwa niaba ya chama na si vinginevyo,” amesema .

Amewataka viongozi hao kutowaachia viongozi wa juu waseme mazuri ambayo yamefanywa na chama na Serikali nao wanatakiwa kwenda kusema kwa wananchi kuhusu utekelezaji wa ilani ya chama ilivyotekelezwa kikamilifu chini ya CCM.

Mjema, ameongeza kuwa historia ya CCM ni kuwakomboa wanyonge, hivyo aliwataka viongozi hao ambao wamepatiwa mafunzo kwenda kusikiliza kero za wananchi kwa maana wananchi wasiposikilizwa watakwenda kusikilizwa kwingine.

Amesema kuwa dhamira ya CCM ni kuendelea kushika ipasavyo hatamu za uongozi na shuguli za umma kwa maslahi ya watanzania na ili suala hilo liendelee kufanikiwa ni vizuri waende kufanya kazi kubwa ya kuzungumza mazuri ambavyo yamefanya chama na kwenda kusimamia miradi ya maendeleo ipasavyo.

Pia amewataka viongozi hao kutoa majibu sahihi kwa wananchi kuhusu mafanikio ambayo yamepatikana kwa kutekelezwa ilani ya chama na kama kuna jambo ambalo hawalijui vizuri wakauliza viongozi kabla ya kutoa majibu ambayo hawana uhakika nao.

No comments:

Post a Comment