
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.
Dkt. Samia Suluhu Hassan, akimsikikiza Mkuu wa Kitengo cha Kilimo Biashara wa
Benki ya NMB - Nsolo Mlozi alipotembelea Banda la Benki hiyo katika maonesho ya
Kimataifa ya Kilimo ya Nane Nane katika viwanja vya John Mwakangale jijini
Mbeya. Wapili kulia ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.
Dkt. Tulia Ackson na Watatu kulia ni Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe.
NA MWANDISH WETU
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameipongeza Benki ya NMB kwa mchango uliotukuka kwenye Sekta ya Kilimo, Uvuvi, Ufugaji na Misitu, sambamba na kusapoti Program ya Kuandaa Vijana na Wanawake Kujenga Kesho Iliyo Bora (BBT).
Mkuu wa Kitengo cha Kilimo Biashara wa Benki ya NMB - Nsolo Mlozi, amemueleza
Mheshimiwa Rais kuwa katika Sekta ya Kilimo (inayojumuisha kilimo chenyewe,
Uvuvi, mifugo na misitu, NMB imeshatoa mikopo ya zaidi ya Shilingi Bilioni 319
tangu Julai 2021 walipoanza kutoa mikopo kwa riba nafuu ya asilimia 9 kwa
mwaka.
Aidha alibainisha kuwa, NMB wameishatoa mikopo ya zaidi ya Shilingi
Trilioni 1.61 katika Sekta ya Kilimo katika kipindi cha miaka sita mfululizo,
huku kwenye Programu ya BBT, tangu Machi wametenga Sh. Bil. 20. Pia, wanatoa
Elimu katika Vituo atamizi kwa vijana na wanawake, ambao wamebeba kaulimbiu ya
maonesho haya ya Nane Nane ambayo wameyadhamini kwa Sh. Milioni 80, huku
wakishirikiana na Wizara ya Kilimo kuwezesha awamu inayofuata wanapoenda kwenye
uzalishaji.
Mlozi alifafanua zaidi kuwa, katika Mikopo ya Kimkakati, NMB imetenga Sh.
Bilioni 20 za mikopo ya ujenzi wa maghala nchi nzima ili kupunguza changamoto
ya uharibifu na upotevu wa mazao ama kuathiri thamani na ubora wa mazao.
Aliongeza kuwa wana mashirikiano na taasisi mbalimbali zinazotoa matrekta
'power tillers,' zana za kilimo na pembejeo, ikiwemo Kampuni ya Agricom Africa.
Kutokana na maelezo hayo Dkt. Samia aliipongeza NMB kwa namna inavyowajali na
kuwathamini wadau wa mnyororo wa thamani wa kilimo, kisha akaiomba benki hiyo
kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali yake katika kuboresha sekta za
kilimo, mifugo, uvuvi na misitu nchini.





No comments:
Post a Comment