BRELA YATAKIWA KUWEZESHA BIASHARA KWA WAJASIRIAMALI WANAWAKE - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Friday, November 24, 2023

BRELA YATAKIWA KUWEZESHA BIASHARA KWA WAJASIRIAMALI WANAWAKE

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila akimkabidhi cheti Ofisa wa  Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Maryglory Mmary, cha kutambua ushiriki wa BRELA  katika Maonesho ya Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi, Wilaya ya Kinondoni katika viwanja vya Biafra wakati wa kufunga  maonesho hayo leo Novemba 24, 2023 jijini Dar es Salaam.

NA MWANDISHI WETU

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila ameitaka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) kuendelea kuwafikia wajasiriamali wanawake ili kuwezesha biashara zao kutambulika kitaifa na kimataifa.

Chalamila ametoa wito huo leo Novemba 24, 2023 wakati  akifunga Maonesho ya Jukwaa la Kuwezesha Wanawake Kiuchumi katika viwanja vya Biafra jijini Dar es Salaam.

Amewataka wajasiriamali wanawake kuchangamkia fursa ya uwepo wa BRELA kwa kurasimisha biashara zao ili  kutambulika kitaifa na kimataifa.

Ameongeza kuwa kwa kurasimisha biashara ni rahisi  kuvuka mipaka  na kuwa na upekee katika soko  ndani na nje ya nchi.

"Uzuri ni kuwa BRELA wapo hapa tumieni fursa hii kupata huduma za sajili mbalimbali  ili iwe rahisi kutambulika na taasisi mbalimbali binafsi na za umma hii itawawezesha pia  kuvuka mpaka wa nchi na kufanya biashara kimataifa", amesema Chalamila.

Pia amewataka BRELA kuendelea kuwafikia wajasiriamali mbalimbali katika Mkoa wa Dar es Salaam na kuwakumbusha umuhimu wa kurasimisha biashara.

Maonesho hayo ya Jukwaa la Kuwezesha Wanawake Kiuchumi Wilaya ya Kinondoni yalianza Novemba 20 na kuhitimishwa leo Novemba 24, 2023.

No comments:

Post a Comment