SERIKALI KUPITIA MKUMBI YAFYEKA TOZO KERO 231 KATI YA 380 - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Thursday, November 16, 2023

SERIKALI KUPITIA MKUMBI YAFYEKA TOZO KERO 231 KATI YA 380

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera na Uratibu wa Bunge, Dkt Jim James Yonazi, akizungumza  kwenye Kikao Maalum cha Kikundi Kazi cha Mazingira ya Biashara jijini Dar es Salaam jana, Dkt. Yonazi . Kulia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa  la Biashara (TNBC), Dkt. Godwill Wanga na Kushoto ni Mwenyekiti Mwenza wa Kikundi Kazi hicho cha Mazingira ya Biashara,Vicent Minja.

NA MWANDISHI WETU

SERIKALI kupitia Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara (MKUMBI) imefuta na kupunguza jumla ya tozo, ada na faini zisizopungua 232 kati ya 380 zinazobainishwa utekelezaji wake sawa na asilimia 61.

Akizungumza Kikao Maalum cha Kikundi Kazi cha Mazingira ya Biashara jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera na Uratibu wa Bunge, Dkt Jim James Yonazi amesema ufutwaji wa tozo, ada na faini hizo ambazo zilikuwa kero kwa ustawi, ukuaji na maendeleo ya biashara na uwekezaji hapa nchini.

“Maamuzi haya yanaonesha dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuifungua Tanzania na kuwa kivutio cha kufanya biashara na uwekezaji,” amesema Dkt. Yonazi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kikundi kazi hicho cha Baraza la Taifa la Biashara(TNBC).

Akielezea zaidi mafanikio yaliyopatikana tangu MKUMBI uanze kutekelezwa, Dkt. Yonazi amesema jumla ya Sheria, Kanuni na Taratibu zipatazo 40 kati ya 88 sawa na asilimia 45.5 zimeshapitiwa na kufanyiwa marekebisho.

“Maboresho haya yote ya Sheria,Kanuni na Taratibu yamesaidia kuchochea ukuaji wa sekta za uchumi hapa nchini zikiwemo sekta za uwekezaji, viwanda na biashara, kilimo, mifugo, afya, maliasili na utalii,” amesema.

Dkt. Yonazi amesema Rais ambaye pia ni Mwenyekiti wa TNBC ameelekeza kuendelea kusimamia utekelezaji stahiki wa MKUMBI sambamba na uhamasishaji wa matumizi ya mifumo yaTeknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kwa lengo la kuongeza ufanisi kwa wafanyabiashara na wawekezaji hapa nchini.

“Nina agiza Wakurugenzi na Idara za Uratibu, Ufuatiliaji na Tathmini pamoja na Maendeleo ya Sekta Binafsi katika Ofisi ya Waziri Mkuu,wafuatilie utekelezaji wa Maazimio ya TNBC na kuwaandikia barua Makatibu Wakuu wote ambao bado hawajawakilisha taarifa za utekelezaji wa maazimio hayo,” amesisitiza Dkt. Yonazi.

Dkt. Yonazi amempongeza Katibu Mtendaji wa TNBC Dkt. Godwill Wanga, watendaji na wafanyakazi wote wa baraza  kwa kazi nzuri na kuwakumbusha wajumbe wote kwenye Kikundi Kazi cha Mazingira ya Biashara kuendelea kufanyia kazi maono na matarajio ya Rais Samia.

Kwa upande wake, Dkt. Wanga amesema Kikosi Kazi cha Mazingira ya Biashara kina jukumu kubwa la kuhakikisha kuwa mazingira ya kufanya biashara yanaendelea kuwa rafiki kwa biashara, uwekezaji na uchumi kwa ujumla na kuvutia uwekezaji kujenga uchumi wan chi.

“Kikundi kazi hiki kina jukumu kubwa la kuondoa na kupunguza  gharama za kufanya biashara na uwekezaji. Hivi hatuna budi kufanya kazi kwa bidii na kuhakikisha tunaandaa na kuwakilisha mapendcekezo yenye tija kwa baraza,” amesema Dkt. Wanga.

Amesema TNBC hufanya kazi kupitia mikutano na vikao katika ngazi mbalimbali kama vile ya Baraza,Kamati Tendaji za Baraza, Mashauriano ya Kiwizara kati ya Sekta Binafsi na Umma(MPPD), Kikosi Kazi cha Kiufundi cha Kiwizara(MTWG), Mikutano ya Baraza la Biashara ngazi ya Mkoa (RBC) na Wilaya (DBC).

No comments:

Post a Comment