NA MAGENDELA HAMISI
CHUO cha Maji kimetakiwa
kuandaa mitaala inayofanikisha wahitimu kupata kazi popote duniani na kuwa na
ufanisi sawa kulingana na mahitaji ya soko la ajira kimataifa na si kujifungia
kwa soko la ndani pekee.
Hayo yamebainishwa leo
Januari 31, 2024 na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Awamu ya
Nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete wakati akifungua maadhimisho ya miaka 50 ya
chuo hicho yanayofikia tamati Februari 2, mwaka huu jijini Dar es Salaam.
“Nashukuru kuona kwamba
mnaushirikiano na vyuo ndani na nje ya nchi hiyo inasaidia kuimarika katika utoaji
wa kozi na wahitimu wanakuwa na soko la ajira popote duniani na si kujifungia
kibongobongo.
“Moja ya changamoto kubwa
katika vyuo vyetu ni kutoa elimu ambayo soko la ajira aihitaji na kusababisha kuwa
na mkusanyika wa watu wanaonung’unika kwamba wao wana digrii lakini kazi hamna
na kusema hii nchi gani?.
“Ukimuuliza umesomea
nini, akikwambia unamuuliza hicho ulichosomea kama ni ajira anakuajili nani,?
nani anayekuhtaji elimu yako,? unakuta hakuna ila amepata sifa kuwa na digrii
ambayo haimsadii, hivyo hakikisheni mitaala yenu inatengeneza watu wanaohitajika
katika soko la ajira,” amesema.
Pia amekitaka chuo hicho
kutumia fedha vizuri wanazopewa na Serikali kwa malengo husika ikiwemo
kukamilisha miradi ya maji na kuimarisha upatikanaji wa maji nchini.
Amesema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan
amejitahidi kuhakikisha kuwa anatekeleza kauli yake ya kumtua Mama Ndoo
kichwani kwa Serikali kutekeleza miradi mingi ya maji.
“Niliwahi kuwa Waziri wa Maji kwa kipindi cha
miaka mitano lakini halikuwa ili ngumu kutokana na kwamba hakukuwa na bajeti ya
kutosha katika sekta hii kulingana na uchumi wetu na baadhi ya wahisani
walisitisha kutupa misaada lakini sasa hali ni shwari, tumieni vuzuri fedha
hizo,” amesisitiza.
Aidha Dkt Kikwete
amekipongeza Chuo cha Maji kwa kuwa na Mfumo wa elimu ambao unawezesha wahitimu
wake kujiajiri au kuajiriwa kwa urahisi zaidi.
“Mfumo wenu wa elimu mnaotumia yaani Competence
Based Approach umesaidia kufanya wahitimu wa Chuo cha Maji kuweza kujiajiri au
kuajiriwa kwa urahisi zaidi hivyo endeleeni kuboresha mazingira ya kufundishia
na kufundisha ili wahitimu waweze kufanya kazi kwa ushindani zaidi ndani na nje
ya nchi” Amesema Dkt. Kikwete.
Naye Mkuu wa Chuo hicho, Dkt. Adam Karia,
ameishukuru Serikali kwa kuendelea kutenga fedha ili chuo kiwezesha kufanya
maboresho mbalimbali na kuleta ufanisi wenye tija





No comments:
Post a Comment