KAMISHNA ADC ATAJA ATHARI ZA MAANDAMANO, AWAKUMBUSHA MWAKA 2001 - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Sunday, January 21, 2024

KAMISHNA ADC ATAJA ATHARI ZA MAANDAMANO, AWAKUMBUSHA MWAKA 2001

   Kamishna Mkuu Taifa wa Chama Cha Alliance For Democratic Change (ADC), Doni Waziri               Mnyamani, akizungumza  na waandishi wa habari hawapo pichani kuhusu maandamano ya Jan 24,2024 ambayo yamehitishwa  na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).


NA MAGENDELA HAMISI

MAANDAMANO ya amani Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ya kuishinikisha Serikali kuondoa miswada minne bungeni wanayodai haina tija imemuibua, Kamishna Mkuu Taifa wa Chama Cha Alliance For Democratic Change (ADC), Doni Waziri Mnyamani.

Akizungumza na jijini Dar es Salaam, Doni amesema kwamba maandamano hayo wahusika wanataka kujipandisha kisiasa ingawa yanaathari kubwa kwa taifa kama ambayo imewahi kutokea Januari 27 2001  

 “Januari 27, 2001 kulifanyika maandano na wakati wa maandalizi yake Januari 25, watu saba wakafariki kabla ya maandamano sasa tuangalie watoto, akina mama, walemavu  ambapo kukitokea vurugu wanakuwa na wakati mgumu kujitetea na athari nyingi zinaweza kutokea na miaka ya nyuma tumeshaziona

“Kwa kweli nina kumbukumbu njema ya maandamano ya mwaka 2001 ambayo yameacha vilio, simanzi na baadhi ya watu wamekuwa walemavu , nafahamu kuandamana ni haki yao kikatiba lakini wanatakiwa kuangalia zinazoweza kujitokeza kwa maslahi mapana ya taifa,” amesema.

Aliongeza kuwa katika kipindi hicho cha mwaka 2001 wengi waliopata athari ikiwemo ya ulemavu hadi leo hawasaidiwi na chama ambacho kilichohitisha maandamano hayo, hivyo hata maandamano ya Januri 24, 2024 kunaweza kujitokeza athari , hivyo wanaopewa ujumbe wa kuandamana wanaweza kutafakari kwanza nani anaweza kuwasaidia wakipatwa na matatizo.

Doni amebainisha kuwa wakati mwingine athari inaweza kumwathiri hata mpita njia na ikasababisha jamii kumdharau kwa kuamini alikuwa kwenye maandamano kumbe sivyo, hivyo maandamano hayo yanaweza kuathiri wasiohusika, ikiwemo wafanyabiashara wadogo kupoteza mitaji yao.

 “Maandamano ya kufa kufaana si maandamano, tunakwenda kuwaumiza watu wasiohusika, nawashauri Chadema wanaweza kufanya maandamano kutokana na kwamba ni haki yao kikatiba lakini athari zake ni kali kwa taifa,” amesema.

Miswada minne ambayo Chadema inataka iondelewa Bungeni licha ya kusomwa kwa mara ya kwanza ni Mswada wa Sheria ya Uchaguzi, Mswada wa gharama za Uchaguzi,Mswada wa Marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa sura ya 258 na Mswada wa Sheria ya Tume ya Uchaguzi wakidai kwamba haina.

MWISHO.

 

.

No comments:

Post a Comment