MAGENDELA HAMISI
ABDUL Nondo amechaguliwa tena kuongoza Ngome ya Vijana ya Chama Cha ACT Wazalendo kwa kupata kura 66 sawa na asilimia 55.4 kati ya 119 ambazo zimepigwa.
Nondo ataongoza Ngome hiyo ya Vijana ya ACT kwa miaka mingine mitano baada ya kupata kura hizo huku mpinzani wake wa karibu, Masabo aliyepata kura 45 sawa na asilimia 37.
Awali akizungumza kabla ya uchaguzi , alitoa wito kwa viongozi watakaochaguliwa wasifumbie macho changamoto zitakazonitokeza katika maeneo yao hususan kuanzia ngazi za vitongoji.
"Asilimia 75 ya Watanzania ni vijana hivyo katika uongozi wenu kwa wale watakaofanikiwa kupata nafasi ya kuongoza hakikisheni amlisahau kundi hilo katika kutatua changamoto zinazowakabiri," amesema.
No comments:
Post a Comment