Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye ni Mbunge wa Kasulu Vijijni, Augustine Vuma, amezungumza hayo leo Machi 27, 2024 mkoani Morogoro kabla ya kurejea Dar es Salaam wakati akitoa majumuisho ya ziara ya ukaguzi wa ujenzi wa reli hiyo na kuangalia majaribio ya usafiri huo unaotarajiwa kuanza safari zake Julai mwaka huu.
NA MAGENDELA
HAMISI
KAMATI ya Kudumu
ya Bunge ya Uwekezaji ya Mitaji ya Umma (PIC), imeridhishwa pasipo na shaka na
mradi wa ujenzi wa reli ya umeme (SGR) kutoka Dar es Salaam, Morogoro hadi
Dodoma na kutoa rai kwa Shirika la Reli Tanzania (TRC), kutunza miundo mbinu ya
reli na kuwasimamia vema wakandarasi ili
wamalize kazi kwa wakati.
Makamu
Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye ni Mbunge wa Kasulu Vijijni, Augustine Vuma, amezungumza
hayo leo Machi 27, 2024 mkoani Morogoro kabla ya kurejea Dar es Salaam wakati akitoa
majumuisho ya ziara ya ukaguzi wa ujenzi wa reli hiyo na kuangalia majaribio ya
usafiri huo unaotarajiwa kuanza safari zake Julai mwaka huu.
“Kamati
tumeridhishwa pasipo na shaka kwamba mradi huu umetenenezwa kwa kiwango cha
stahiki na unavutia kwa watanzania na tumeelezwa pindi ukikamilika utakuwa na
faida nyingi kwa maana tayati umetoa ajira za moja kwa moja 30,000 na zisizo za
moja kwa moja 150, 000 ambazo zimewezesha kipato cha shilingi bilioni 350.
“Pia
tumeambiwa safari zitakapoanza zitapunguza nusu ya muda wa kusafiri unaotumika
na mabasi kutoka Dar es Salaam, Morogoro hadi Dodoma na tunaamini Watanzania
watatumia muda mfupi katika safari na kusafirisha mizigo na tunaona kabisha
inakwenda kufanikiwa,” amesema.
Ameongeza
kuwa kutokana na hatua ambayo imefikiwa ya ujenzi na majaribio ya safari kwa
niaba ya kamati hiyo anaipongeza Serikali chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan
kwa kazi kubwa ambayo imefanyika na kutoa fedha kwa ajili ya mradi huo ambao
unaonekana unakwenda kuwa na faida kubwa kwa taifa na wananchi kwa ujumla.
Pia
aliipongeza TRC kwa usimamizi mzuri wa ujenzi wa mradi huo ambao upo katika
hatua za mwisho kukamilika kwa njia ya Dar es Salaam Morogoro hadi Dodoma na
dhahiri Julai safari zitaanza kama ambavyo Rais Dkt Samia ameagiza.
Ameongeza
kuwa hadi kukamilika kwa mradi huo, Serikali itakuwa imetumia Dola million 10
sawa na sh. trillion 23 za kitanzania na tayari imetumia asilimia 40 ya fedha
hizo na kutoa rai kwa watanzania kutumia fursa ya uwepo wa reli hiyo kibiashara
itakayowaongezea kipato kwa kusafirisha mizigo kwa bei nafuu.
Naye
Mwenyekiti wa Bodi TRC, Ally Kalavina kutokana na mradi huo ulipofikia na
watakiwa katika majaribio ya safari kutoka Dar hadi Morogoro ni dhahiri
watatekeleza maagizo ya Rais Dkt Samia kwa wakati ifikapo Julai kwa safari
kuanza rasmi ya kubeba abiria na mizigo, Dar es Salaam kwenda Dodoma.
“Vitu vingi
vimekamilika yaliyobaki ni maeneo madogo ambayo yanaendelea kufanyiwa kazi ili
kuhakikisha yanakamilika kwa wakati uliopangwa na niwaondoe hofu Watanzania
kuwa wawe na amani kwani tren zitaanza kufanya kazi kwa wakati,” amesema.
Pia
Mkurugenzi wa TRC, Masanja Kadogosa
amesema wanaishukuru kamati hiyo kwa kukagua ujenzi na huo na majaribio na
kuridhishwa na hatua ambayo imefikiwa kwa sasa na kusisitiza kuwa mchakato wa
nauli upo chini Mamlaka ya Udhibiti Usafari wa Ardhini (LATRA) na kabla ya
Julai zitatangazwa kwa wananchi.
“Kwa upande
wetu tumeshakamilisha michakato inayotuhuu na hatua iliyobaki ni kwa Latra
ambayo tayari wameshafanya majadilino na baadhi ya wadau na pindi
watakapokalisha watatangaza nauli kabla ya Julai,” amesema.
Mkurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Masanja Kadogosa (kulia) akiwa na Mwenyekiti wa Bodi TRC, Ally Kalavina kwenye treni ya umeme (SGR) wakienda Morogoro kutokea Dar es Salaam.






No comments:
Post a Comment