BRELA YATOA MAFUNZO KUHUSU DHANA YA MILIKI MANUFAA ARUSHA - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Saturday, May 30, 2026

BRELA YATOA MAFUNZO KUHUSU DHANA YA MILIKI MANUFAA ARUSHA

 


NA MWANDISHI WETU

DHANA ya Miliki Manufaa (Beneficial Ownership) iliyoanza kutumika rasmi mwaka 2022, imeendelea kuwa nguzo muhimu katika mfumo wa usajili wa kampuni nchini Tanzania, ikilenga kuongeza uwazi katika umiliki wa biashara na kudhibiti mianya ya utakatishaji fedha pamoja na udanganyifu wa kifedha.


Kwa mujibu wa Meneja wa Kampuni kutoka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Harvey Kombe, wakati wa mafunzo ya Miliki Manufaa yaliyofanyika jijini Arusha, alisema bado kuna changamoto kubwa ya usahihi wa taarifa zinazowasilishwa kwenye mfumo wa usajili wa kampuni. Alibainisha kuwa takribani asilimia 85 % ya maombi yanayowasilishwa katika mfumo huo huwa na makosa, hali inayotokana na kutofuatwa kwa taratibu sahihi za ujazaji wa taarifa za miliki manufaa.


Katika mazingira hayo, imekuwa ikisisitizwa kuwa mawakili na wahasibu wana nafasi muhimu ya kuhakikisha taarifa za wamiliki halisi wa kampuni zinakaguliwa kwa umakini kabla ya kuwasilishwa, ili kupunguza kiwango cha makosa yanayojitokeza katika mfumo.


Mafunzo hayo hufanyika katika mikoa mbalimbali yenye shughuli kubwa za kiuchumi na mwitikio mkubwa wa usajili wa kampuni, ambapo Arusha ni miongoni mwa maeneo ambayo BRELA hupokea maombi mengi ya Miliki Manufaa.


Kwa ujumla, hatua hiyo ni sehemu ya jitihada zinazoendelea za kuboresha mfumo wa usajili wa kampuni nchini, huku msisitizo ukiwekwa katika kuhakikisha taarifa za miliki manufaa zinakuwa sahihi, zenye uhalisia na zinazoweza kusaidia kuimarisha uwazi na uwajibikaji katika sekta ya biashara.


Mafunzo hayo yamekuwa na matokeo chanya kwa taasisi na wadau wake, kwani yamechangia kuongeza uelewa, kuboresha usahihi wa taarifa zinazowasilishwa, na kupunguza makosa katika mfumo wa usajili wa kampuni.





No comments:

Post a Comment