WITO umetolewa kwa wanafuika ambao wamepata huduma kutoka Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), kutoa mrejesho ili taasisi hiyo iweze kuimarisha kiutendaji na kuwachukulia hatua maofisa wake wanaokiuka maadili.
Sophia Mtakasimba ambaye ni Ofisa Mawasiliano katika Mfuko huo, ametoa wito huo Mei 25 wakati semina kwa Waandishi wa Habari ambao ni wanachama wa Jumuia ya Wafanyakazi wa Vyombo vya Habari Tanzania (JOWUTA) iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Akifafanua hilo, Mtakasimba amesema , kurejesha mrejesho kuna umuhimu mkubwa kwani inasaidia taasisi kuboresha huduma ili kila anayehudumiwa aone anajaliwa.
Pia amesisitiza hata suala la rushwa likitokea Kwa anayehudumiwa ni vizuri kulitolea taarifa ili hatua zichukuliwe kwa muhusika na si vema kulipeleka kwenye mitandao ya kijamii ambako inaweza kuchukua muda zaidi kufanyiwa kazi.
"Ni vizuri wanufaika wakatumia mifumo rasmi ya kutoa maoni kuhusu kero wanazopitia ili tuchukue hatua na si vizuri kuzipeleka kwenye mitandao ya kijamii kwani huko kunaichafua Serikali," amesema.









No comments:
Post a Comment