IKIWA MFIDIWA HAJARIDHIKA NA MALIPO YAKE ANATAKIWA KUKATA RUFAA - MWANASHERIA WCF - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Monday, May 25, 2026

IKIWA MFIDIWA HAJARIDHIKA NA MALIPO YAKE ANATAKIWA KUKATA RUFAA - MWANASHERIA WCF



 NA MWANDISHI WETU

IMEELEZWA kwamba mfanyakazi ambaye ni mwanachama wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), ikiwa hakuridhika na malipo ya fidia anatakiwa kukata rufaa ili apate haki stahiki.

Hayo yameelezwa leo, Mei 25 jijini Dar es Salaam na Ofisa Sheria Mwandamizi wa mfuko huo, Janeth Mgoma wakati wa warsha ya kuwajengea uwezo wanachama wa Jumuia ya Wafanyakazi wa Vyombo vya Habari Tanzania (JOWUTA).


Mgoma amefafanua kwamba ikiwa mfidiwa hakuridhika na malipo aliyolipwa baada ya kupata ajali akiwa kazini, anachotakiwa kufanya ni kukata rufaa kwa Mkurugenzi wa WCF.


Aidha ameongeza kuwa ikiwa pia hatoridhika na maamuzi ya rufaa  iliyotolewa na Mkurugenzi,  atapaswa kukata tena ndani ya siku 30 kwa waziri mwenye dhamana na ikiwa bado hajarishika atatakiwa kwenda mahakamani kwa hatua zaidi ya kudai haki yake.

"Hizo ndizo hatua ambazo mfidiwa wa malipo ya kuumia kazini atatakiwa kuzifuata ikiwa hajaridhika na malipo yake, naamini akifuata mchakato huo stahiki zake atazipata,"amesema.






No comments:

Post a Comment