KERO ZA MUUNGANO ZAKARIBIA KUMALIZIKA - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Tuesday, March 26, 2024

KERO ZA MUUNGANO ZAKARIBIA KUMALIZIKA


NA AHMED SAGAFF, MAELEZO

TAKRIBAN kero nne ambazo zimebakia katika Muungano wa Tanganyika na Zanzibar unaofikisha miaka 60 zinaendelea kupatiwa ufumbuzi.


Akizungumza leo jijini Dodoma, Waziri wa Nchi - Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Dkt. Suleiman Jafo amesema jitihada za kutatua kero hizo zimeimarika katika uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.


Dkt. Jafo amezitaja kero hizo kuwa ni mgawanyo wa mapato yatokanayo na hisa za Serikali ya Mapinduzi ha Zanzibar zilizokuwa katika Bodi ya Sarafu ya Afrika Mashariki.


Nyingine ni mgawanyo wa faida kutoka Benki Kuu, na uingizwaji wa sukari inayozalishwa katika kiwanda cha Mahonda katika soko la Tanzania Bara.


"Ufanisi umekuwa mkubwa sana. Nilitoa takwimu hapo mwanzo kwamba kipindi hiki tumeweza kutatua takribani kero 15 za muungano. Hili si jambo dogo kwa kipindi cha miaka mitatu kuweza kufanikisha," amearifu Dkt. Jafo.


Naye, Msemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi amefahamisha kuwa Watanzania wanajivunia historia ya Taifa lao katika miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ulioasisiwa Aprili 26, 1994.


"Natoa wito kwa waandishi wa habari na kuwaomba ushirikiano wenu katika kipindi hiki cha maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano," ameomba Ndg. Matinyi.


Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imekuwa ikichukua jitihada za kuimarisha muungano imara wa serikali mbili kwa kupunguza kero kuliko kukubali maoni ya muungano wa serikali tatu ambao una madhara mengi yanayoweza kusababisha kuligawa Taifa na kuwagawa Watanzania.

No comments:

Post a Comment