NA MAGENDELA HAMISI
JUMUIYA za kiraia zinazoendesha shughuli mbalimbali nchini zikiwemo za kidini, kitamadumi na nyinginezo zimetakiwa kufuata taratibu na sheria ili kulinasua taifa katika nchi zinazohitaji ufuatiliaji wa karibu Enhanced Monitoring (Grey List).
Hayo yamezungumzwa leo jijini Dar es Salaam Machi 26,2024 na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhandisi Hamad Masauni, wakati wa uzinduzi wa kampeni ya usajili jumuiya za kiraia nchini.
"Kutokana na kuwepo changamoto ya baadhi jumuiya za kiraia kuripotiwa kutumika kufanikisha kutenda makosa ya jinai ikiwemo utakatishaji fedha, ufadhili wa shughuli za kigaidi, usafirishaji haramu wa binadamu na biashara haramu ya siraha nchi imeingizwa kwenye Grey List" amesema.
Ameongeza kuwa licha ya taifa kuingizwa katika kundi hilo, pia wadau wa maendeleo wamepewa tahadhari hiyo kushindwa kusimamia jumuiya hizo jambo ambalo linahitaji uwepo kwa ushirikiano wa pamoja kudhibiti hilo.
Pia katika uzinduzi huo, amewataka Makatibu Tawala , viongozi Kamati za Usalama, Watendaji Kata kuhakikisha kufuatilia jumuiya hizo ili kudhibiti ambazo zinakwenda kinyume na Sheria na taratibu za nchi.
Pia amewatoa wito kwa jumuiya zinazohitaji kusajiliwa au kupewa msaada wa aina yoyote zipewe huduma hiyo haraka bila kwenda kushughulikia mahitaji yao jijini dodoma.
Pia Katibu MKuu wa Wizara hiyo, Ally Gugu amesema watashirikiana kuhakikisha jumuiya hizo zinafuata Sheria na taratibu , a nchi ili kudumisha amani na utulivu uliopo nchini.
Aliongeza kuwa uzinduzi wa kampeni ya usajili wa jumuiya hizo utasaidia kukua takwimu sahihi ya jumuiya zilizopo na namna kizisimamia ipasavyo.
Kwa upande wake msajili wa jumuiya za Kiraia, Emmanuel Kihampa amesema lengo la kampeni hiyo ni kuhamasisha usajili wa vikundi mbalimbali ili kulinda maslahi ya wanachama na chama chenyewe au taasisi hali itakayoongeza amani kwa nchi na kuifanya nchi izidi kuvutia uwekezaji.
Amesema sambamba na kutambuliwa serikali imeweka utaratibu wa kuwawezesha ili waweze kujiendeleza kiuchumi kwa maslahi ya nchi.
"Serikali imeona tufanye zoezi hili ili kuwezesha nchi yetu kutoka kwenye kundi la ambalo tumewekwa ambalo linaweza kuleta changamoto katika kuvutia uwekezaji,Nchi imewekwa kwenye kundi la nchi zinazotakiwa kufuatiliwa kwa karibu na taasisi ya kimataifa",Amesema.
Aidha ametoa rai kwa wadau kuja kuwekeza nchini kwani nchi ina amani na usalama.
.jpeg)




No comments:
Post a Comment