BABA LEVO APEWA UBALOZI KAMPUNI YA INARA CERAMIC - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Wednesday, April 3, 2024

BABA LEVO APEWA UBALOZI KAMPUNI YA INARA CERAMIC


NA MAGENDELA HAMISI

MSANII wa muziki wa kizazi kipya maarufu Kwa jina Baba Levo amepewa ubalozi wa kutangaza tiles za Kampuni ya INARA CERAMIC kutoka nchini India.

Akizungumza mbele ya waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Baba Levo, amesema ameamua kujiunga na Inara Ceramic kutokana na kampuni hiyo kutokana ubora wao katika kutengeneza tiles kimataifa.

"Nina furaha kusaini mkataba wa miezi sita na baada ya hapo kama nitafanya vema nitaongezewa mkataba wa miaka mitatu," amesema.

Pia ameshawauri watu mbalimbali wanaofanya ujenzi kuhakikisha wanatumia tiles original kutoka Kampuni hiyo kutoka I dia.

Wakati huo huo ameahidi kwa wateja watakaonunua tiles na zikiharika ndani ya miezi sita zikiharibika watarudishwa kiwandani kupata nyingine.

Naye, Mkurugenzi wa kampuni hiyo Manam Mody, amesema kuwa anaamini kujiunga Baba Levo naamini watafanya vema na kufika mbali.

 

No comments:

Post a Comment