RAIS DK.MWINYI AHIMIZA NIDHAMU, UADILIFU NA MSHIKAMANO - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Saturday, April 6, 2024

RAIS DK.MWINYI AHIMIZA NIDHAMU, UADILIFU NA MSHIKAMANO


NA MWANDISHI WETU

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk.Hussein Ali Mwinyi amehimiza suala la nidhamu, maadili, uwajibikaji, uadilifu, mshikamano, umoja na upendo baina ya viongozi na watendaji wa Serikali katika kutenda haki kwa wananchi. 


Amesema hayo katika Kongamano la Kiimani kwa Viongozi na Watendaji Wakuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar lililoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais na kuratibiwa na Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar ukumbi wa Idrissa Abdul-Wakil Kikwajuni, Mkoa wa Mjini Magharibi Aprili 6, 2024.


Aidha Rais Dk.Mwinyi amesema suala la nidhamu sio kwa Majeshi peke yake ni suala la utumishi wa umma mzima.


Kwa upande mwingine Rais Dk.Mwinyi amesema ili kuwepo uwajibikaji , maadili na nidhamu jambo kubwa ni kuwa na hofu ya Mungu na kuchunga ahadi zinazotolewa ili kutekeleza wajibu kwa uadilifu. 


Rais Dk.Mwinyi amesema kongamano lijalo waalikwe Wenza wa viongozi na watendaji wa Serikali ili wapate kujifunza mada zinazotolewa na Masheikh na Wahadhiri. 


Vilevile Rais Dk.Mwinyi amesema kodi ndiyo inayoendesha Serikali kwa kutekeleza huduma mbalimbali za kijamii , suala la kulipa kodi ni halali .








No comments:

Post a Comment