SOMBI: SERIKALI IMETENGA SH. BILIONI 100 KUJENGA VYUO VYA VETA NCHINI - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Saturday, April 27, 2024

SOMBI: SERIKALI IMETENGA SH. BILIONI 100 KUJENGA VYUO VYA VETA NCHINI

 Makamu Mwenyekiti  wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, MNEC Rehema Sombi, akizungumza katika mahafari ya 18 ya Chuo Cha Furahika kilichopo, Buguruni Malapa Ilala jijini Dar es Salaam, kulia ni Mwenyekiti wa Vijana CCM (W) Ilala, Juma Mizungu.

 NA MAGENDELA HAMISI

SERIKALI imetenga shilingi bilioni 100 kwa ajili ya kujenga vyuo vya VETA katika Halmashauri 63 kwenye mikoa isiyokuwa na mikoa ambayo haina vyuo hivyo kwa ajili ya kutoa fursa kwa vijana kupata elimu ya ufundi ili kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kutengeneza ajira ya kujiali ama kuajiliwa.

Hayo yamesemwa leo, Aprili 27, 2024 na jijini Dar es Salaam na Makamu Mwenyekiti  wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, MNEC Rehema Sombi, wakati wa mahafari ya 18 ya Chuo cha Furahika kilichopo Buguruni Malapa na kufafanua kuwa fedha hizo zinakwenda kwenye Halmashauri 63 katika mikoa isiyo na vyuo hivyo.

Chuo hicho kilichoanzishwa mwaka 2021 na kupatiwa usajili namba na VET/DSM/PR/2021/D169 kikiwa na wanafunzi wawili na hadi sasa kimefanikiwa kutoa vijana zaidi ya 400 katika fani tofauti ambao wamefanya vema na kupata ajira katika hoteli na mashirika mbalimbali nchini na Serikalini.

“Mimi ni mtoto Ilala na niliwaambia mkiwa na jambo lolote niko tayari kushirikiana nanyi kama ambavyo leo, nitaendelea kuwa balozi wenu ili kuunga mkono juhudi ya Rais, Dkt Samia Suluhu Hassan katika nyanja ya eilimu, jambo hili la kutoa elimu bure linatekeleza Ilani ya CCM ya mwaka 2020/2025,” amesema.

Katika mahafari hayo ya 18, MNEC Sombi alichangia fedha kwa ajili ya kununua cherehani mbili iliyopokelewa na Mwenyekiti wa Vijana, CCM( W ) Ilala, Juma Mizungu, zitazotumika kwa kufundishia wanafunzi wa fani ya ushonaji wanaojiunga na chuo hicho na kuahidi kuwafikia wahisani ili wakisaidie vifaa vya TEHAMA kama vile kompyuta.

MNEC Sombi katika mahafari hayo alitoa wito kwa wahitimu kuzingatia nidhamu wanapokwenda na kuwa na subra wakati wa kusubiri ajira ili wasijiingize katika tabia ovu ikiwemo uhuni na matumizi ta dawa za kulevya zitakazoharibu ndoto zao.

Naye Mkuu wa Chuo hicho Dkt David Msuya, amesema kwa sasa wanaendelea na ujenzi wa chuo chao kilichopo Kinyerezi jijini Dar es Salaam na kuwaomba wahisani kujitokeza ili kumalizia ujenzi huo utakawapunguzia  adha ya kulipa kodi.

“Tunatumia fedha nyingi kwa ajili ya kulipa kodi ambayo wakati tunalipatukiwa na wanafunzi wachache na imekuwa ni changamoto kwetu hivyo tunawaomba wazazi na walezi kuleta vijana wao katika programu hii ya elimu bure itakayowasaidia kujikwamua kiuchumi,” amesema.

Ameongeza kuwa wanatoa elimu kwa ngazi ya diploma kwa miaka miwili kwa kozi ya hoteli na nyinginezo na kwa msimu ujao unaoanza Mei mwaka huu wataanza kutoa elimu kwa njia ya mtandao 'Online' kwa wahitaji na mwanafunzi atafika chuoni hapo kwa ajili ya kufanya mitihani ya mwisho tu.

 

Pia alimpongeza Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt Hussein Mwinyi kutokana na Kamisheni ya Utalii, kupokea wanafunzi wa chuo hicho na wengine kuwapa ajira jambo linalosaidia kutimiza ndoto zao vijana wanaotoka chuoni hapo kuondokana na utegemezi na kuwasaidia familia zao.

  Kushoto ni Mkuu wa Chuo, Dkt David Msuya akizungumza katika mahafari hayo.

No comments:

Post a Comment