TABORA UNITED YAIFUATA KIBABE SINGIDA FOUNTAIN GATE - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Tuesday, April 2, 2024

TABORA UNITED YAIFUATA KIBABE SINGIDA FOUNTAIN GATE

Christina Mwagala, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano Tabora United. 

NA MWANDISHI WETU


KIKOSI cha wachezaji 22 ,Viongozi pamoja na Benchi la ufundi wa Timu ya  Tabora United kimeondoka jeo kwenda jijini Mwanza kwa ajili ya mchezo wa michuano ya Kombe la Azam Sports Federation ASFC dhidi ya Singida Fountain Gate.


Tabora United itakuwa ugenini katika mchezo huo wa mtoano ikiwa ni hatua ya 16 bora, ambao utapigwa Alhamisi ya Aprili 04 katika Uwanja wa CCM Kirumba Jijini hapo na kwamba maandalizi yanaendelea kufanyika kwa ustadi mkubwa.


Kikosi hicho cha Nyuki wa Tabora chini ya Kocha Mkuu Denis Goavec kabla ya kuondoka hapo asubuhi kutakuwa na program ya mazoezi na kwamba badae  mchana safari ya kuelekea Jijini Mwanza itaanza.


" Tumekuwa na kipindi bora cha kufanya mazoezi Chini ya Kocha Goavec na wachezaji wametimiza kile walichokuwa wanalekeza, hatuna changamoto kila kitu kinakwenda vizuri , hivyo kila mmoja yupo tayari kwa safari.


Tunakwenda kucheza na Singida Fountain Gate ambao tunajua kabisa ni wazuri ,wanabenchi nzuri la ufundi pia wana wachezaji wazuri ila tutapambana kuhakikisha kuwa  tunaendelea kwenye hatua inayofuata ya michuano hiyo ya ASFC. 


"Hata hivyo kwa upande wa Afya za wachezaji wote vizuri na morali nzuri ingawa tutamkosa Cletus Emotan ambaye anasumbuliwa na majeraha na kwamba ataungana na wenzake mara baada ya kurejea kutoka Jijini Mwanza," alisema. 


No comments:

Post a Comment