DK.MWINYI AHIMIZA KUDUMISHA AMANI NA UMOJA - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Friday, May 3, 2024

DK.MWINYI AHIMIZA KUDUMISHA AMANI NA UMOJA


NA MWANDISHI WETU, ZANZIBAR

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi  amehimiza kudumisha amani utulivu, umoja na mshikamano  kuzidi kupiga hatua ya maendeleo nchini.


Rais Dk.Mwinyi amesema hayo alipojumuika na Waumini wa Dini ya Kiislamu katika  Sala ya Ijumaa Msikiti wa Mbuyuni , Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi tarehe 03 Mei 2024.


Aidha Rais Dk.Mwinyi amewataka Waumini waendelee kuiombea nchi na viongozi  wake ili kutekeleza ahadi walizoahidi.






No comments:

Post a Comment