MGANGA MKUU WA SERIKALI YA SIERRA LEONE NA TIMU YA WATAALAMU WA AFYA WAMETEMBELEA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA TEMEKE - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Friday, May 3, 2024

MGANGA MKUU WA SERIKALI YA SIERRA LEONE NA TIMU YA WATAALAMU WA AFYA WAMETEMBELEA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA TEMEKE


 NA MWANDISHI WETU


MGANGA wa Mkuu wa Serikali ya Sierra Leone, Dkt. Sartie Kenneh na timu ya wataalamu wa afya kutoka wizara ya afya ya nchini humo ametembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke (TRRH) kwa lengo la kujifunza namna Tanzania inavyosimamia mfumo wa manunuzi na uendeshaji wa huduma za kifamasia nchini.

 Katika ziara hiyo, Dkt. Kenneh  na timu yake walipata fursa ya kutembelea maeneo ya hospitali ikiwemo na madirisha mbalimbali ya dawa yaliyopo katika hospitali, jengo la CT -Scan na wodi mpya ya usafishaji damu.  

 

Akizungumza mara baada ya ziara hiyo, Dkt. Kenneh amesema amefurahishwa  na mfumo mzima wa uendeshaji wa manunuzi wa dawa uliopo  na  namna ulivyoaungana moja kwa moja na wizara ya afya kupitia MSD. 

Pia amefurahishwa  na huduma za rufaa zinazotolewa na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke kusema kuwa amejifunza mambo mengi 

 

Kwa upande wake, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke, Dkt. Joseph Kimaro ameeleza namna timu hiyo kutoka sierra leone ilivyojifunza na kupendezwa na maswala mbalimbali katika uendeshaji wa huduma za afya hasa katika huduma za rufaa. 

Aidha Dkt. Kimaro ameeleza kuwa kwa sasa Hospitali inahuduma nzuri za rufaa kutokana na uwepo wa magari manne ya kubebea wagonjwa hivyo kurahisisha usafirishaji wa wagonjwa wa rufaa kutoka kituo cha afya kimoja hadi kingine. 

 

Mfamasia kutoka idara ya vifaa tiba(MSD), Suzana Majule, amesema kuwa ziara hiyo imekua nzuri kwa wageni kwani  wameweza kujifunza mengi katika ngazi ya rufaa ya mkoa.

Pia amesema kuwa uhusuiano wa mbili hizo  umezidi kuimarisha ushirikiano katika masuala ya ununuzi na ugavi inchi.









No comments:

Post a Comment